Social Icons

Alhamisi, 8 Mei 2014

Adhabu waliyopewa Villareal kwa tukio la Dani Alves kutupiwa ndizi

Ligi kuu ya Hispania (LFP) imeipa adhabu klabu ya Villareal kutokana na kosa la shabiki wao kumfanyia vitendo vya kibaguzi mchezaji wa FC Barcelona mbrazil Dani Alves.
LFP imeiadhibu Villareal kwa faini ya 12,000 euros ($16,000) ambazo ni zaidi ya milioni 25 za Kitanzania baada ya mmoja wa mashabiki wao kumtupia ndizi beki huyo wa Barcelona kwenye game ya timu hizo iliyopigwa El Madrigal.
Ni tukio ambalo lilichukua headlines mpaka kufanya watu wengi wakiwemo mastaa Samuel Eto’o, Luis Suarez na wengine kupiga picha wakiwa wanakula ndizi kuonyesha kupingana na matukio ya ubaguzi wa rangi.
Shabiki huyo wa Villareal tayari kafungiwa maisha na klabu hiyo kwenda uwanjani kuangalia mpira ambapo pia siku kadhaa baada ya hili tukio alikamatwa na Polisi ambao hata hivyo hawakutaka kumuonyesha hadharani kutokana na kuepuka kuhatarisha maisha yake.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates