Social Icons

Alhamisi, 8 Mei 2014

RONALDO: NEYMAR ANAWEZA KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA

400997_heroa
CRISTIANO Ronaldo anaamini kuwa nyota wa Barcelona, Mbrazil, Neymar atakuwa mchezaji bora wa dunia.
Wakatalunya walimsajili kinda huyo mwenye miaka 22 kutoka klabu ya Santos ya Brazil kwa dau linalokadiriwa kuwa paundi million 87.2 na amefunga mabao 9 katika mechi za ligi na kutoa pasi za mwisho 8 katika mechi zake 25 alizocheza.
Licha ya Rea Madrid kuwa wapinzani wakubwa kutafuta ubingwa wa La Liga kuliko Barcelona, Ronaldo anadhani kuwa nyota huyo wa Brazil atakuwa moja ya wachezaji nyota zaidi duniani.
“Namtazama Neymara kama mchezaji mkubwa,” aliwaambia SportsTVnews. “ Nadhani kwa kipindi cha sasa ameonesha kuwa atakuwa mchezaji mkubwa kwa baadaye”.
“Alichelewa kufiti katika mfumo wa Barcelona kiuchezaji, alikuwa na matatizo mwanzoni, lakini sina wasiwasi juu ya yeye kuwa mchezaji bora wa dunia au bora zaidi na zaidi”.
Ronaldo mwenye miaka ya 29 alipoulizwa hatima ya timu ya taifa ya Ureno kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil alikiri kuwa nchi yake imepangwa kundi ngumu zaidi na timu za Ujerumani, Ghana na Marekani.
“Sisi hatupewi nafasi kubwa,” alisema. “Lakini tutajitahidi kulifurahia. Tunajua tupo kundi gumu, kwa maoni yangu ni kundi lenye mataifa makubwa zaidi duniani”. 
“Tunatakiwa kwenda hatua kwa hatua. Tutakuwa na mchezo mgumu wa kwanza dhidi ya Ujerumani, halafu tutacheza na Ghana na kumalizia na Marekani. Baada ya hapo tutaona”.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates