Timu ya soka ya Taifa ya Australia, maarufu kama ‘ Soccerrose’ ndiyo timu inayoshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo mmoja duniani. Australia waliichapa, American Samoa magoli 31-0, April 11, 2001 katika mchezo wa kimataifa unaotambuli wa na FIFA…Soccerrose, walitua nchini, Brazil siku ya juzi tayari kwa michuano ya kombe la dunia inayotaraji kuanza kutimua vumbi, juni 12. Australia ipo katika kundi la pili sambamba na mabingwa watetezi, Hispania, makamu bingwa wa fainali zilizopita, Uholanzi, na Chile.
Kikosi cha kocha, Ange Postecoglou kimeshawahi kucheza michuano hiyo mara tatu na mafanikio yao makubwa ni kufika hatua ya 16 bora, mwaka 2006… Kwa mara ya kwanza, Australia, ilifuzu kwa fainali za mwaka 1974 zilizofanyika nchini Ujerumani na kuondoka patupu.
Walipata suluhu-tasa dhidi ya Chile, kisha wakapoteza kwa waliokuwa wenyeji wa michuano, Ujerumani Mashariki, na Ujerumani Magharibi na kuondoshwa mashindanoni pasipo kufunga goli lotote.
Ikiwategemea zaidi wachezaji wake wazoefu kama Tim Cahiil, na nahodha wa kikosi hicho, Michael Jadinak ambaye anakipiga katika kikosi cha Crystal Palece ya England ,kikosi hicho kimekuwa timu ya kwanza kuwasili,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni