Social Icons

Alhamisi, 22 Mei 2014

CHAMA CHA MAPINDUZI CHATEMBELEWA NA UJUMBE KUTOKA NRA UGANDA HII LEO

Naibu Katibu Mkuu akizungumza na Ugeni Kutoka chama rafiki cha National Resistence Army Kutoka Uganda waliofika Kujifunza Mambo mbalimbali ya Kiuongozi/Kiutendaji ndani ya Chama cha Mapinduzi.Naibu katibu Mkuu CCM-Bara Mh:Mwigulu akimkabidhi Kitabu/cha
Mwongozo cha Chama cha Mapinduzi Kiongozi wa Serikali ya Uganda(NRA).Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara Mh:Mwigulu Nchemba akimkabidhi Katiba Ndugu Nnsiima Emmanuel Bigirwa Mchambuzi wa Mambo ya Siasa Kutoka Serikali ya Uganda.Mh:Mwigulu akimkabidhi kanuni za Uchaguzi zinazotumiwa na Chama cha Mapinduzi.
 Ujumbe huu Kutoka NRA Wakifurahia Jambo kutoka Chama Cha Mapinduzi.Viongozi hawa Kutoka Uganda Wamefurahia sana Kupata Elimu ya namna Chama cha Mapinduzi kinavyojiendesha,Ikumbukwe Uganda kwa Muda mrefu imekuwa Ikiendesha siasa zake katika Mfumo wa Chama Kimoja,Ujio wa Vyama Vya Upinzani umekuwa Changamoto kwa chama cha NRA hivyo wanatumia fursa mbalimbali Kujifunza namna ya Kufanya siasa za Ushindani kama CCM inavyofanya hapa Tanzania.Upande wa Kulia ni Hon. Nabulya Ssentongo Theopista.Mh:Mwigulu Nchemba akipokea Zawadi Kutoka Ujumbe wa Chama cha NRA-Uganda.Mh:Mwigulu Nchemba akitoa Maelezo namna Chama cha Mapinduzi kinavyofanya Kazi zake na Muundo wa Uongozi Kuanzia Ngazi ya Shina hadi Tawi na Mfumo Mzima wa Uchaguzi unavyoendeshwa ndani ya Chama cha Mapinduzi.
Hafla hii imefungua Mlango Mkubwa zaidi wa Urafiki na Umoja kati ya Chama cha Mapinduzi na Chama Kinachoongoza Serikali ya Uganda cha National Resistence Army Kutokana na Kuwekeana Malengo ya Kuendelea Kushirikiana Katika Uga wa Siasa na Nyanja zingine za Kiuchumi na Kijamii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates