Social Icons

Jumanne, 13 Mei 2014

kuelekea brazukaa hembu soma hiii........aaaaa

MBRAZILI AJIFAFANISHA NA OSAMA ILI AINGIZE PESA

Osama wa Brazili akionesha baadhi ya picha alizopiga na watu maarufu.
Osama wa Brazil akiwa katika eneo lake la kupigia picha na wateja.
Osama feki akiwa ndani ya mgahawa wa Rock and Roll alioajiriwa.
Sao Paolo, Brazil
Mgahawa mmoja nchini BrazilI, Rock and Roll umeamua kumtumia mtu ambaye amefanana kwa kila kitu na aliyekuwa gaidi namba moja duniani, Osama Bin Laden kama kivutio kimojawapo pindi fainali za kombe la dunia zitakapoanza.
Jamaa huyo aliyejulikana kwa jina la Ceara Francisco mpaka sasa amekuwa kivutio na ataendelea kuvutia hasa mashabiki wa timu ya England pindi watakapowasili.
Wazo la kufungua mgahawa huo na kumuweka Bin Laden feki limetokana na tukio ambalo lilijiri nchini Marekani, tarehe 9 ya mwezi wa 11 ambapo gaidi huyo alifanya shambulio  kutafutwa kila pembe ya dunia.
Hata hivyo katika mgahawa huo inaelezwa zaidi ukitaka kufika unaambiwa Osama anapatikana pande hizo na unapiga naye picha kadhaa ambazo huzihifadhi kama kumbukumbu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates