Social Icons

Jumamosi, 10 Mei 2014

Giggs anena ujio wa kocha mpya asema ................


Kaimu mkufunzi wa timu ya Manchester United nchini Uingereza, Ryan Giggs amesema kuwa hasikitishwi na hatua ya kumtafuta kocha mpya wa kilabu hiyo .
Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal ambaye anaitaka kazi hiyo anatarajiwa kuteuliwa kama mrithi wa aliyekuwa mkufunzi wa timu hiyo David Moyes.

Wakati huohuo mshambulizi wa kilabu ya Manchester United Wayne Rooney yuko tayari kuonyesha uhodari wake katika michuano ya kombe la dunia.Giggs aliteuliwa kama kaimu kocha wa kilabu ya Manchester United baada ya Moyes kutimuliwa kutokana na msururu wa matokeo mabaya mnamo mwezi Aprili.

Kulinga na kaimu meneja wa kilabu yake Ryan Giggs,Rooney ameshindwa kung'ara katika michuano mingi ya kimataifa tangu alipoanza kusakata soka ya kiwango hicho katika mechi za kuwania taji la ubingwa wa ulaya mnamo mwaka 2004.
Hatahivyo Giggs ana imani kwamba Rooney ataiwakilisha vyema Uingereza katika dimba la dunia nchini Brazil.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates