Social Icons

Jumamosi, 31 Mei 2014

DZEKO 2,DROGBA 1,BOSNIA-HERZEGOVINA YAI VURUGA IVORY COAST MECHI YA KIRAFIKI KUEREKEA BRAZUKA.







TIMU YA TAIFA YA ENGLAND YATIKISA ENGLAND...

No chance: Peru keeper Raul Fernandez clutches at thin air as Welbeck's shot flies into the net
Get in: Skipper Steven Gerrard was one of the first to congratulate Sturridge after his screamer

MBEYA; MUME AUA MKE KIKATILI



MWANAMKE aliyetambuliwa kwa jina la Christina Hayola(35), mkazi wa Kijiji cha Lwalanje, alikutwa amekufa na mwili wake kubainika kuwa ulikuwa na majeraha ya kukatwa katwa Kifuani, kichwani na mguu wake wa kulia.
 
Unyama huo unadaiwa kufanywa na mumewe, Mussa Nsagaje, maarufu kwa jina la Mwaulambo, kwa kile kinachodaiwa kuwa chanzo ni ugomvi wa masuala ya wivu wa kimahusiano(Ngono) ulioanzia eneo la kilabu cha pombe.
 
Mwili wa marehemu ulikutwa katika Kijiji cha Magamba, kata ya Isansa, tarafa ya Igamba, wilayani Mbozi, mkoani Mbeya na mtuhumiwa alitoroka baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Ijumaa, 30 Mei 2014

WABUNGE WA KAMBI RASMI YA UPINZANI WASUSIA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI NA KUTOKA NJE YA BUNGE


Kiongozi  wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe amewatoa wabunge wote wa upinzani Bungeni ikiwa ni shinikizo la kuipinga Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kama ilivyokuwa imewasilishwa na Waziri wa Wizara hiyo Professa Sospeter Muhongo.

 
"Hatuwezi kuendelea kuzungumzia bajeti ya Serikali isiyokuwa na sera,mimi kama Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni siwezi kuendelea kuiongoza kambi inayoburuzwa," amesema Mbowe na kuongeza:
 
"Tunawaachia bungeni lenu mpitishe bajeti yenu ili siku zijazo mkutane na hasira za wananchi,kwakuwa haya mlishayapanga".

ASERNE WENGER KUSAINI MKATABA WA MIAKA MITATU ASERNAL NA KULAMBA PAUNDI 24


File photo dated 18/05/2014 of Arsenal manager Arsene Wenger celebrating outside the Emirates Stadium during the FA Cup winners parade in London. PRESS ASSOCIATION Photo. Issue date: Monday May 19, 2014. Manager Arsene Wenger admits he would always question whether Arsenal were on the right path during nine barren seasons, but now hopes people will focus on the positives following their FA Cup triumph at Wembley. See PA story SOCCER Arsenal. Photo credit should read: Anthony Devlin/PA Wire
Amepumua: Arsene Wenger akishangilia baada ya kumaliza ukame wa miaka 9 bila kombe mwezi huu baada ya kutwaa taji la FA.
Big challenge: Wenger must now turn his FA Cup winners into Premier League champions
 Chagamoto kubwa: Wenger kwa sasa anahitaji kupeleka nguvu za FA katika michuano ya ligi kuu.
ASERNE Wenger atasaini mkataba mpya wa miaka mitatu na Asernal siku chache zijazo baada ya kukubaliana na vipengelea vya mkataba huo ambao utamuweka katika klabu hiyo mpaka mwaka 2017.
Wenger alimaliza hofu ya kuondoka klabuni hapo majira ya kiangazi mwaka huu baada ya kufuta ukame wa miaka 9 bila kombe kufuatia kutwaa `ndoo` ya kombe la FA. 
Kulikuwa na hoja kuwa kama kocha huyo mwenye miaka 64 angeshindwa kumaliza ukame wa miaka 9 bila kombe Emirates basi angefutiwa kazi yake, lakini Wenger alionesha maarifa yake Wembley baada ya kuitwanga 3-2 Hull na kujihakikishia maisha London kaskazini.
 Arsenal  wamempatia Wenger mkataba wenye thamani ya paundi milioni 24 na paundi milioni 100 kwa ajili ya usajili.
Mtandao wa  Sportsmail unafahamu kuwa Wenger atasaini mkataba unaompatia paundi milioni 8 kwa kila msimu.
Na atapewa bajeti kubwa zaidi katika historia ya Asernal ili kumsaidia kushinda taji la ligi kuu msimu ujao kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004.
Finally... Wenger gets his hands on the trophy at Wembley for the first time since 2005
 Mwisho wa siku Wenger alishika kombe mkononi mwake katika uwanja wa Wembley kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2005

MATOKEO YA UCHAGUZI MALAWI KUTANGAZWA HIVI PUNDE ,POLISI WATUMIA MABOMU KUTULIVU VURUGU MMOJA AFA


Wakati  tume ya uchanguzi nchini Malawi inataraji kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais nchini humo hivi punde ,zimezuka vurugu kubwa kati ya makundi yanayomuunga mkono Rais Joyce Banda na wapinzani wake.

Imeelezwa  kuwa katika  vurugu  hizo zilizozuka mchana wa leo polisi  wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya  wananchi hao na kumna taarifa  ya mtu mmoja  kupoteza maisha kutokana na vurugu  hizo.

Duru  za kisiasa  kutoka nchini Malawi zinadai kuwa  hali ya amani kwa  sasa nchini  humu si swari kutokana na vurugu  hizo ambapo watu kadhaa wanaripotiwa  kujeruhiwa  vibaya na kukimbizwa Hospital kwa matibabu  zaidi

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA NCHI WASHIRIKA WA MAENDELEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akibadilishana mawazo na mabalozi na wawakilishi wa nchi washirika wa maendeleo kabla ya  mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia  michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika  kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa saba kutoka kushoto) akiwa katika mazungumzo  na mabalozi na wawakilishi wan chi washirika wa maendeleo katika mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia  michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika  kutekeleza  Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)

HII NDIO TIMU YA KWANZA KUWASILI BRAZUKA.....


Australia-National-Football-Team-3 
Timu ya soka ya Taifa ya Australia, maarufu kama ‘ Soccerrose’ ndiyo timu inayoshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo mmoja duniani. Australia waliichapa, American Samoa magoli 31-0, April 11, 2001 katika mchezo wa kimataifa unaotambuli wa na FIFA…Soccerrose, walitua nchini, Brazil siku ya juzi  tayari kwa michuano ya kombe la dunia inayotaraji kuanza kutimua vumbi, juni 12.  Australia ipo katika kundi la pili sambamba na mabingwa watetezi, Hispania, makamu bingwa wa fainali zilizopita, Uholanzi, na Chile.

Kikosi cha kocha, Ange Postecoglou kimeshawahi kucheza michuano hiyo mara tatu na mafanikio yao makubwa ni kufika hatua ya 16 bora, mwaka 2006… Kwa mara ya kwanza, Australia, ilifuzu kwa fainali za mwaka 1974 zilizofanyika nchini Ujerumani na kuondoka patupu. 
Walipata suluhu-tasa dhidi ya Chile, kisha wakapoteza kwa waliokuwa wenyeji wa michuano, Ujerumani Mashariki, na Ujerumani Magharibi na kuondoshwa mashindanoni pasipo kufunga goli lotote. 
Ikiwategemea zaidi wachezaji wake wazoefu kama Tim Cahiil, na nahodha wa kikosi hicho, Michael Jadinak ambaye anakipiga katika kikosi cha Crystal Palece ya England ,kikosi hicho kimekuwa timu ya kwanza kuwasili, 

TANAPA NA NSSF WATOA UFAFANUZI DHIDI YA TUHUMA ZA CHADEMA KWA ZITTO KABWE


Baada  ya msemaji  wa   kambi  ya  Upinzani  Bungeni  ambaye  ni  waziri  kivuli  wa  wizara  ya  Habari,Michezo, Vijana  na  utamaduni  kumtuhumu  Zitto  Kabwe   kuhusika  na  kinachoitwa  ufisadi  katika  shirika  la  TANAPA  na  NSSF, mashirika  haya  yameamua  kutoa  ufafanuzi  kuhusiana  na  tuhuma  hizi  ili  kuweka  mambo  sawa......

Meneja Uhusiano wa TANAPA, Paschal Shelutete  ameliambia  gazeti  la  Mwananchi  toleo  la  leo ( May 30)  kuwa    shirika  hilo  linakitambua  kiasi  hicho  kilichotajwa  na  wapinzani  na  kwamba  fedha  hizo  zilikuwa  ni  malipo  ya  wasanii  wa   Leka Dutigite   ambao  walifanya  kazi  ya  kuitangaza   Hifadhi ya Saadan...

“Leka Dutigite ilifika Hifadhi ya Saadan na kuitangaza kupitia kazi za sanaa... sikumbuki ni lini lakini walifanya kazi na DvD zake zipo. 

“Ifahamike si Leka Dutigite pekee, tunafanya kazi na wasanii mbalimbali kutangaza vivutio, mbuga na hifadhi zetu,” Shelutete  ameliambia  gazeti  la  Mwananchi


Naye  Meneja Kiongozi wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume ameliambia  gazeti  hilo  kuwa pesa walizozitoa kwa kundi hilo zilikuwa malipo ya kutengenezea wimbo maalumu wa shirika hilo na nyingine ni za udhamini wa onyesho lililofanyika mwaka jana mkoani Tanga.
 
“Kweli mara ya kwanza tuliwalipa Sh25 milioni wasanii wa kundi hilo ili watutengenezee wimbo na Sh56 milioni zilikuwa za udhamini wa onyesho lao, lakini kwa masharti ya kututangaza jambo ambalo lilikuwa na mafanikio kwetu kwani tumefanikiwa kupata wateja wapya 30,000 kutoka sekta isiyo rasmi,” alisema Chiume.
 
Alisisitiza kuwa wametumia kiwango hicho cha pesa ili kujitangaza kwa kuwa hata mashirika ya kijamii yanapaswa kufanya hivyo ili kuvutia wateja wengi zaidi.

PICHA ZA RAY C AKIWA MTAANI LEO, KUHAMASISHA MATEJA KUACHA UNGA


 
Leo Ray C Foundation tuliwatembelea waathirika wa madawa ya kulevya Kinondoni!!!
nimeongea nao sana na kuwahamasisha waje kupata Tiba ya Methadone Mwananyamala....
nimefurahisana kuskia kutoka Kwao kwamba na wao wamechoka na Maisha ya utumwa......
Tuko pamoja nao kuhakikisha tunawasaidia.......


Ray C Foundation Pamoja inawezekana... 

TAARIFA YA SUMATRA YA KUHAMISHA KITUO CHA DALADALA MWENGE - MAKUMBUSHO


Wamiliki, madereva na abiria wote mnatangaziwa kuwa kituo cha daladala Mwenge kitafungwa rasmi siku ya Jumapili jioni tarehe 01.06.2014. Kuanzia siku ya jumatatu asubuhi tarehe 02.06.2014 kituo kitakachokuwa kinatumika ni Makumbusho tu.
  
Sababu kubwa ya kufunga kituo hicho ni ufinyu wa eneo hilo jambo linalochangia dadalada kushindwa kuingia kituoni kwa wakati hasa vipindi vya asubuhi na jioni hivyo kusababaisha foleni kubwa katika eneo la Mwenge.
  
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa eneo hilo kwa sasa litabaki kuwa eneo la wazi.
  
Madereva mnatakiwa kutii agizo hili ili kuepukana na hatua kali ambazo zitachukuliwa dhidi ya yeyote ambae atakaidi, aidha abiria mnatakiwa msilazimishe kushushwa eneo ambalo hakuna kituo cha daladala.
  
Barabara za kuingia na kutoka kituoni Makumbusho zinaendelea kukarabatiwa na Manispaa ya Kinondoni ili kusiwe na tatizo la kuingia kituoni hapo.
  
Conrad Shio
Afisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki

Jumatano, 28 Mei 2014

HILI NDILO GAUNI ALILO VAA KIM KARDASHIAN WAKATI WA HARUSI YAKE.....


MMILIKI WA MAN UNITED AFARIKI DUNIA

 Malcolm Glazer, aliyeshinda tenda ya utata ya kuichukua Manchester United mwaka 2005, amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 85.
Mfanyabiashara huyo wa Marekani atakumbukwa kama bilionea wa Florida aliyeichukua kuimiliki binafsi United miaka tisa iliyopita na kuwekeza zaidi ya Pauni Milioni 500. 
Glazer mkubwa amekuwa mgonjwa kwa muda sasa na kuwaachia shughuli za uendeshaji wa United watoto wake wa kiume, Joel na Avram. 
Mmiliki: Malcolm Glazer amefariki akiwa na umri wa miaka 85

Msemaji wa United amesema: "Fikra za kila mmoja katika United zipo kwa familia usiku huu,".
Familia ya Glazer bado wanamiliki Tampa Bay Buccaneers, timu ya mpira wa miguu ya Marekani waliyoinunua mwaka 1995. Na kwenye tovuti ya Bucs, ambako zimetangazwa habari za kifo cha Glazer.

Jumanne, 27 Mei 2014

NA HII NDIO EVANC BUKUKU COMEDY SHOW SI MCHEZO.......CHEKI PIX......

 MCHEKESHAJI SIDE STORY
 EVANC BUKUKU UKITOA SHOW HATARI........

 ONE THE ONE AND 2 DJ CAUSE OR ONAVIEWS.BLOG
 ENIKA AKITOA MUSIC COMEDY
 ENIKA NA BANANA(NDIZI).


 MCHEKESHAJI DOGO PEPE
 DADA ANGALIA MBAVU ZISIVUNJIKE
MCHEKESHAJI MAGANIKO..........HATARIIIII
 MDADA NAYE HAKUWA NYUMA AKAENDA TOA JOKE

 
 RAY MCHEKESHAJI AKIFANYA YAKE.

BRAZIL WAFANYIWA VIPIMO, TAYARI KWA WORLD CUP.......


















Jeshi la Nigeria limebaini walikofichwa wasichana waliotekwa

Jeshi la nchini Nigeria limesema linajua mahali walikofichwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa wakiwa shuleni lakini hawawezi kuitaja sehemu hiyo hadharani. 


Wasichana hao walitekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo linadai haliwezi kuwaachia hadi watakapobadilishana wafungwa wao na serikali ya nchi hiyo. 

 

Kwenye kituo cha TV cha Nigeria, imetangazwa kwamba japo imefahamika walipo Wasichana hao ambao bado wanashikiliwa mateka….. majeshi ya Nigeria na mengine yanayoendesha opareshen hiyo hayatotumia nguvu za kijeshi kwenye uokoaji wa wasichana hawa. 

Kitendo cha kutekwa kwa wasichana hao kimeibua majonzi makubwa miongoni mwa wazazi na kufanya kuibuka kwa kampeni iliyosambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari yenye jina la Bring Back Our Girls ikimaanisha “Rudisheni wasichana wetu”

 
 
Blogger Templates