Flaviana Matata siku ya jumatano tarehe 21 May alijumuika na wananchi wengine mkoani Mwanza katika Ibada maalum ya kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuwaombea marehemu waliopoteza maisha yao baada ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba miaka 18 iliyopitta.
Flaviana Matata ni Miss Universe Tanzania 2007 ambapo pia ni Mwanamitindo wa Kimataifa akifanyia shughuli zake nchini Uingereza na Marekani yeye ni mmoja wa wahanga waliopoteza ndugu zao kwenye ajali hiyo ambapo yeye alimpoteza mama yakemzazi na Kaka yake. Mbali na kusindikizwa na ndugu jamaa na marafiki pia alisindikizwa na aliyekuwa Balozi wa marekani Mwanaidi Maajar
Ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba ilitokea katika ziwa Victoria mnamo tarehe 21/5/1996 na kupoteza maisha ya zaidi yawatu 1000, Ukiondoa mrembo huyo Misa hiyo pia itahudhuliwa na Sheikh kutoka ofisi ya sheikh mkuu wa mkoa, Wachungaji wa kanisa kwa ajili ya kuendesha ibada maalum, ndugu wa karibu wa Flaviana akiwemo baba yake Mzazi, Marafiki zake, wananchi mbalimbali napia Viongozi wa serikali kupitia kampuni ya Marine Services Company Limited. Ambapo wadau kutoka Dar es Salaam wamesafiri leo asubuhi kwa udhamini mkuu wa shilika la ndege laFast Jet.
Ibada hiyo fupi itafanyika katika makaburi ya Igoma ambapo ndipo walipozikwa na tukio hilo kama kawaida litaambatana na shughuli ya kuweka mashada ya maua na kuwasha mishumaa.Hafla hii inaendeshwa kwa ushikiano wa karibu kutoka katika kampuni ya Marine Services ambapo wamekua wakitupa ushirikiano mzuri kwa miaka yote hii. Safari ya kwenda Mwanza
Flaviana na Balozi Mwanaidi Maajar walishiriki kuweka mashada katika mababuri
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ambwene Yesaya almaarufu kama AY alikuwepo kuungana na Flaviana Matata
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni