SAMUEL Eto`o ametajwa katika kikosi cha awali cha wachezaji 28 cha timu ya taifa ya Cameroon kwa ajili ya fainali za kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil.
Kocha Volker Finke amemuita Eto`o na kumfanya nyota huyo wa Chelsea acheze fainali zake za nne za kombe la dunia.
Eto`o alicheza fainali za kwanza za kombe la dunia mwaka 1998, akaja kucheza 2002 na 2010 nchini Afrika kusini, na kama atacheza fainali za mwaka huu basi nyota huyo mwenye miaka 33 atafikia rekodi ya Rigobert Song na Jacques Songo, ambao waliichezea Cameroon katika fainali nne za kombe la dunia.
Eto`o ambaye alitangaza kustaafu soka la kimataifa mwaka jana, lakini akabadilisha maamuzi yake pia anatarajia kufikia rekodi ya mabao ya Roger Milla.
Nyota huyo wa zamani wa Cameroon alifunga mabao 5 katika fainali zote za kombe la dunia alizoichezea nchi yake, lakini Eto`o amefunga mabao mawili tu katika fainali tatu alizocheza.
Cameroon wataanza kampeni za kombe la dunia kwa kuvaana na Mexico juni 14 kabla ya kukutana na Croatia na wenyeji Brazil waliopo kundi A.
Kikosi cha awali cha wachezaji 28 cha timu ya taifa ya Cameroon kwa ajili ya kombe la dunia hiki hapa;
Walinda mlango: Loic Feudjou (Coton Sport), Charles Itandje (Konyaspor), Sammy N’Djock (Fethiyespor), Guy N’dy Assembe (Guingamp).
Walinzi: Benoit Assou-Ekotto (QPR), Henri Bedimo (Lyon), Gaetan Bong (Olympiacos), Aurelien Chedjou (Galatasaray), Cedric Djeugou (Coton Sport), Jean-Armel Kana-Biyik (Rennes), Nicolas N’Koulou (Marseille), Dany Nounkeu (Besiktas), Allan Nyom (Granada).
Viungo: Eyong Enoh (Antalyaspor), Raoul Loe (Osasuna), Jean Makoun (Rennes), Joel Matip (Schalke), Stephane Mbia (Sevila), Landry N’Guemo (Bordeaux), Edgar Salli (Lens), Alex Song (Barcelona).
Washambuliaji: Vincent Aboubakar (Lorient), Maxim Choupo-Moting (Mainz), Samuel Eto’o (Chelsea), Mohammadou Idrissou (Kaiserslautern), Benjamin Moukandjo Nancy), Fabrice Olinga (Zulte Waregem), Pierre Webo (Fenerbahce).
On standby: Frank Bagnack (Barcelona), Zock Bep (Cosmos de Bafia).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni