Sifa kwa wanasiasa kokote duniani ni nadra, hasa kwenye mitandao ya kijamii, lakini watu wamemmiminia sifa Rais wa Uruguay baadhi wakitamani kama marais wao wangekuwa kama Rais Jose Mujica wa Uruguay.
Kwenye Twitter kuna zaidi ya ujumbe laki moja wa watu nchini Uhispania wakitamani kama waziri mkuu wao angekuwa kama Rais Maskini zaidi duniani Jose Mujica wa Uruguay.
Rais huyo anasifika kwa kuendesha gari kuu kuu , kuishi maisha ya watu wa kawaida na sehemu kubwa ya mshahara wake yeye hupatia mashirika ya misaaada ya kibinadamu...kiasi kwamba anajulikana kama Rais masikini zaidi duniani.
Na ndio maana waziri mkuu wa
Hispania Mariano Rajoy huenda asifurahie sana kufananishwa na Rais wa Uruguay.
Lakini swali ni watu wangapi duniani wanaweza kufananisha Rais Uruguay na marais wao? Ni Marais wangapi duniani wanatoa mishahara yao kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu, kuishi maisha ya kawaida na kuendesha gari lililochoka?
Baadhi ya wananchi wanahoji kwa nini nchi kama Uruguay ambayo haina uchumi mkubwa ina huduma bora zaidi kwa jamii kuliko Hispania ambayo imekomaa kiuchumi wakati rais wake hana uchu wa madaraka na tamaa ya pesa?
Mitandao ya kijamii hutumiwa sana kwa mijadala kama hii. Swali ni je nani ana jambo zuri la kusema kumhusu Rais wake hasa katika hizi nchi zetu za Afrika? Unadhani kiongozi yupi barani Afrika anaweza kufananishwa na huyu Rais wa Uruguay? Je kuna Rais asiyeishi maisha ya kifahari enzi hizi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni