Social Icons

Jumatano, 30 Aprili 2014

Baada ya Didier Kavumbagu,DUMAYO asaini Azam,ANGALIA PICHA AKISAINI.

Timu ya Azam bado inaendelea na usajili wake wa wachezaji ambapo baada ya Didier Kavumbagu aliyekua akiichezea Yanga kupewa mkataba wa mwaka mmoja, sasa wamemuongeza mchezaji mwingine kikosini Azam FC.

IMG-20140430-WA0003
Frank Domayo ndio kiungo mpya aliyesainiwa na Azam Fc kwa mkataba wa miaka miwili na kujiunga na mabingwa wapya wa Tanzania Bara.

MASUPA STAA WABONGO NAO WALA NDIZI KUKEMEA UBAGUZI.

Screen Shot 2014-04-30 at 6.02.00 PM
Screen Shot 2014-04-30 at 5.12.47 PM

TAZAMA PICHA- MKUTANO WA UKAWA KATIKA VIWANJA VYA KIBANDA MAITI MJINI UNGUJA, ZANZIBAR JANA


Viongozi wa Wajumbe wa kundi la UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) ndani ya Bunge Malaum la Katiba, wamehutubia maelfu ya watu waliohudhuria mkutano wao katika viwanja vya Kibanda Maiti mjini Unguja, Zanzibar jioni ya leo.
 

Kwa mujibu wa Katibu wa UKAWA ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, kesho mkutano mwingine wa UKAWA unatarajiwa kufanyika Pemba kabla ya mikutano kama hiyo kuendelea katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara/Tanganyika kama vile Dar es Salaam, Kigoma, Morogoro, Mwanza, Iringa, Arusha n.k. 

Mtatiro amesema lengo la mikutano hiyo ni kuwaelimisha wananchi juu ya hatua yao ya kuondoka Bungeni na kususia vikao vya Bunge Maalum la Katiba na kile wanachoamini kinapaswa kufanyika.
 
 

TUZO NANE ZA SOUTH AFRIKA MUZIKI AWARD ZAENDA KWA MAFIKIZOLO(KHONA).

 
Wasanii wanaounda kundi la muziki la mafikizolo kutoka Afrika ya Kusini.

Kundi la muziki kutoka Afrika ya Kusini limeshinda tuzo nane ambazo zinajulika kama “South Africa Muzic Award”

Hili ni moja ya kundi ambalo limeshawahi kufanya show kadhaa nchini Tanzania, ambapo onesho la moja lilifanyika Mliman City mwezi uliopita.

Miongoni mwa vipengele walivyoshinda ni pamoja na album ya mwaka, kundi bora. 


Wasanii wengine waliopata tuzo hizo jana usiku ni pamoja na Zahara, Kabomo, Nakhane Toure, Ifan Big Nuz, Micasa muziki na wengine

KAMA WEW NI MSHABIKI WA WANA JANGWANI:-KAVUMBAGU ASAINI AZAM MWAKA MMOJA

Didier Kavumbagu akiwa na Viongozi wa timu ya Azam Fc. 
Hans Mloli na Sweetbert Lukonge
UKISUSA sisi twala! Hivyo ndiyo Azam wanavyoweza kusema baada ya kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu.
Kavumbagu alimaliza mkataba na Yanga baada ya msimu uliomalizika hivi karibuni na Yanga hawakufanya naye mazungumzo yoyote, hali iliyoonekana kuwa walikuwa wakisita kumpa mkataba mpya.
Mshambuliaji wa Azam, Didier Kavumbagu akikamilisha kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
Straika huyo ambaye alimaliza msimu akiwa ameifungia Yanga mabao 11, yakiwa ni nane pungufu ya aliyekuwa kinara, Mrundi mwenzake Amissi Tambwe wa Simba, alikuwa hajui hatima yake baada ya ligi kumalizika.
Azam wameamua kutumia mwanya huo kwa kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja jana alasiri, kisha wakatulia kama vile hawajui kinachoendelea.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika ndani ya Azam, mshambuliaji huyo baada ya kusaini mkataba, atarudi kwao kwa ajili ya mapumziko kabla ya kurejea kuanza maandalizi ya msimu mpya na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara, mwezi mmoja baadaye.
“Kweli Kavumbagu amesaini mkataba wa mwaka mmoja na timu yetu, ni jambo ambalo uongozi hautaki kulitangaza kwa sasa kuepuka kuvuruga mambo, lakini ukweli ndiyo huo,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina.
Chanzo kingine kilicho ndani ya timu hiyo, nacho kililithibitishia Championi Jumatano kuwa, mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja.

Paparazi ilimtafuta Katibu Mkuu wa Azam, Nassor Idrissa lakini simu yake haikuwa ikipatikana. Naye mwenyekiti wa klabu hiyo, Said Mohammed hakuwa tayari kuzungumza kwa undani kuhusiana na ishu hiyo.
“Kawaida yetu tukisajili mchezaji yeyote huwa tunaita waandishi wa habari, kwa hiyo subirini, kama ni kweli tutawaita tulizungumzie suala hilo,” alisema Mohammed kisha akakata simu bila kuhitaji kufafanua zaidi.
Usajili huo, unamaanisha kwamba, ushindani wa namba katika safu ya ushambuliaji ya Azam utaongezeka na huenda timu hiyo ikawa na moja ya safu za ushambuliaji kali zaidi kwenye Ligi Kuu Bara.

Tayari Azam ina mastraika wengine hatari wakiongozwa na Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast, John Bocco, Gaudence Mwaikimba na Mganda, Brian Umony. Azam FC wanajiandaa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Picha za watu 14 maarufu wakila ndizi kupinga ishu ya Dani Alves

.
davido
TZA SAMUEL ETOO VITA DHIDI YA UBAGUZI WA RANGI
Screen Shot 2014-04-30 at 1.58.22 PM
Screen Shot 2014-04-30 at 1.58.36 PM
Screen Shot 2014-04-30 at 1.58.53 PM
Screen Shot 2014-04-30 at 1.59.24 PM
Screen Shot 2014-04-30 at 1.59.32 PMScreen Shot 2014-04-30 at 2.16.05 PMScreen Shot 2014-04-30 at 2.15.54 PMScreen Shot 2014-04-30 at 2.15.44 PMScreen Shot 2014-04-30 at 2.15.31 PMScreen Shot 2014-04-30 at 2.15.21 PMScreen Shot 2014-04-30 at 2.15.10 PMScreen Shot 2014-04-30 at 2.14.57 PM

BASI LA AM COACH LAPATA AJALI ENEO LA IPULI NA KUSABASHA KIFO CHA MWANAFUNZI MMOJA KUFARIKI HAPO HAPO.


 
Askari Polisi Kitengo cha usalama barabarani wakiuchukua mwili wa mtoto aliyegongwa na basi la kampuni ya A.M maeneo ya Ipuli Mnadani ambalo lilikuwa likitokea jijini Mwanza,katika ajali hiyo watu kadhaa wamejeruhiwa.

Umati mkubwa wa watu ambao ulifiika kushuhudia ajali hiyo mbaya

Maafisa wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Tabora walifika eneo la tukio na kusaidia majeruhi wa ajali hiyo.

Wananchi wakishuhudia mwili wa mtoto aliyegongwa na basi hilo ambapo walishauri Serikali iliifungie kampuni hiyo ya A.M Coach kuleta mabasi mkoani Tabora ambayo walidai kuwa ni mabovu na yanausalama mdogo kwa wasafiri.

 
Huu ndio uskani wa basi hilo ni mbovu kupindukia na si salama kwa kutumika  kwenye magari ya usafirishaji wa binadamu

Kufuatia kutokea kwa ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na mabasi ya kampuni ya A.M,wananchi mkoani Tabora wameiomba Serikali kuyapiga marufuku mabasi ya kampuni hiyo kwakuwa yamebainika kuwa ni mabovu na si salama kwa wasafiri na wapita njia.

Wananchi hao ambao walifika katika moja ya tukio la ajali iliyotokea eneo la Ipuli mnadani kushuhudia ambapo wanafunzi wawili waliokuwa wakienda shuleni kwa ajili ya masomo kwa muda wa ziada,mwanafunzi mmoja alifariki papo hapo na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na basi la A.M Coach lenye nambari za usajili T 861 ATZ lililokuwa likifanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Tabora.

Aidha wananchi hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao wamedai kuwa mabasi ya kampuni hiyo yamekuwa yakiingia mjini kwa kasi kubwa huku yakionekana kuyumba barabarani na kuzidi kutia shaka hata watumiaji wa barabara kuu za mkoa wa Tabora.


Wameitahadharisha Serikali kuwa endapo watayaachia mabasi hayo huenda yatasababisha ajali mbaya zaidi na hata vifo visivyo vya lazima. 

Yule tajiri Mmarekani aliesema hataki watu Weusi kapewa hii adhabu

Screen Shot 2014-04-30 at 3.30.29 AM
NBA imesema kutokana na uchunguzi kukamilika kuhusu mmiliki wa timu ya Los Angeles Clippers Donald Sterling dhidi ya maneno ya kibaguzi kwa watu weusi, imempa kifungo cha maisha mmiliki huyo mwenye umri wa miaka 80.

Wanasema baada ya kufanya uchunguzi Donald amekubali kwamba sauti iliyosikika ikitoa maneno mazito ya kibaguzi dhidi ya watu weusi ni ya kwake ambapo alikua akiongea na Mwanamke anaedaiwa kuwa mpenzi wake.
Donald ambae aliwahi kukiri siku kadhaa zilizopita kwamba hatoiuza hii timu, kwenye adhabu ya maisha aliyopewa ni kwamba hatoruhusiwa kuhudhuria mazoezi ya timu yake wala kwenda kwenye game zote maishani mwake na vilevile hatoruhusiwa kufanya maamuzi yoyote kwenye timu.
Screen Shot 2014-04-30 at 3.35.06 AM
Kingine kilichoongezeka ni faini ya dola za Kimarekani milioni 2.5 ambazo kibongobongo inagonga kwenye 4107500000 ambapo inasemekama hii sauti ya Sterling akitoa maneno ya kibaguzi ilirekodiwa September 2013 na kwamba alishtukia kwamba karekodiwa.

Yote haya yametokana na kuvuja kwa sauti ya mazungumzo kati yake na girlfriend ambapo Donald Sterling aliongea maneno makali ya kibaguzi kwa kusema kwamba hataki girlfriend wake ajihusishe na watu weusi kwa kupiga picha au kwenda nao kwenye mechi.
Imeshangaza zaidi kwa sababu timu yake ina wachezaji mashuhuri weusi kama Chris Paul na Blake Griffin aliyewahi kucheza ligi ya chuo pamoja na Mtanzania Hasheem Thabeet lakini wakiwa wanatoka kwenye vyuo tofauti.
Kamishna wa NBA amesema atatumia nguvu ya uongozi wake kuhakikisha L.A Clippers haimilikiwi tena na Donald Sterling.

Screen Shot 2014-04-30 at 3.27.39 AMScreen Shot 2014-04-30 at 3.27.31 AM

MAGAZETI YA LEO JUMATANO 30/04/2014















ACHA MUNGU AITWE MUNGU MWILI MMOJA VICHWA VIWILI.

MAAJABU YA 

Mapacha hawa wanaitwa Abby na Brittany wamezaliwa mwaka 7/3/1990 nchini MAREKANI. 
Mapacha hawa wameungana mwili na kuwa mwili mmoja wenye vichwa viwili, lakina chakushangaza zaidi kila mmoja anamfumo wake wa kupumua na moyo wake na maini yake,
Vitu wanavyo changia ni mwili mmoja ikiwemo miguu miwili na mikono miwili.



 
 
Blogger Templates