Social Icons

Jumanne, 27 Mei 2014

MSANII RACHEL HAULE WA BONGO MOVI AFARIKI DUNIA!


Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.
Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi zitawajia baadae.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates