Social Icons

Jumamosi, 29 Novemba 2014

AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JIJINI DAR:

 

Helikopta ya Maliasili (TANAPA) imedondoka maeneo ya Kipunguni, jijini Dar na kuua watu wote watano wakiwemo rubani na Polisi.


BUNGE LAHIRISHWA TENA ASUBUHI HII

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Anna Makinda Amelazimika Kuliahirisha Bunge Asubuhi Kwa mara ya Pili   mara baada ya Kuliahirisha Saa tatu Asubuhi Hadi saa Kumi Jioni  .
Hali hiyo Imetokana na Mazungumzo yanayoendelea kwajili ya Wabunge Kuridhiana Maendekezo ya Kamati ya PAC yaliyokuwa yanataka Baadhi ya Viongozi Kuwajibika.Hali iliyosababisha Bunge hilo kutokuelewana la Kulazimika Kuhairishwa jana Saa nne Usiku.

Jumanne, 25 Novemba 2014

MAISHAAA NA PESA


My Weather 

mzigo
Kumbe sio Dar peke yake haya mabo ya kuweka pesa na kupiga nayo picha, kila sehemu haya sasa Floyd MyWeather kazitandaza

DR.SLAA AKIWA NYUMBANI KWAKE.

Dk   Slaa  akiwa  nyumbani  kwake  pamoja na  wanafamila   wengine

Dk  SLAA  akiendelea  na  maongezi  na  wanafamila  akiwa nyumbani  kwake
DK   SLAA  akicheka  baada  ya  mtoto  wake  kumfurahisaha 
Hapa  Slaa akiongea  na  mgeni  wake

Waandamanaji wafanya vurugu St.Louis

Mji wa St Louis limeshuhudia maandamano na vitendo vya uporaji baada ya jaji kupitisha uamuzi wa kumshtaki aliyemuua kijana mweusi Michael Brown.
Polisi mjini humo wamesema vurugu zimeleta madhara makubwa zaidi kuliko ya mwezi Agosti baada ya kuuawa kwa kijana huyo.
Kamanda wa Polisi wa St Louis, Jon Belmar amesema alisikia milio ya risasi takriban 150 kutoka kwenye makundi ya watu.
Brown alifyatuliwa risasi na Polisi tarehe 9 Mwezi Agosti, hali iliyoibua ghadhabu na maandamano.
Watu wengi wa jamii ya Afrika na Marekani walitoa wito wakitaka Afisa Polisi Darren Wilson ashtakiwe kwa mauaji.
Rais wa Marekani Barack Obama alitoa wito kwa wamarekani kuwa watulivu na kukubali maamuzi ya Jaji kuhusu kesi hiyo.

Miili yatelekezwa Sierra Leone

Wafanyakazi ambao huzika miili ya Watu waliokufa kwa Ebola, mjini Kenema nchini Sierra Leone wamegoma kwa sababu hawajalipwa marupurupu yao.
Miili 15,kati ya hiyo mingi inahitajika kuzikwa,imetelekezwa katika hospitali kuu mjini humo.
Mwili mmoja unadaiwa kutelekezwa kwenye Ofisi ya Meneja wa Hospitali hiyo, huku miili miwili ikiwa imetelekezwa kwenye mlango wa kuingilia Hospitali hapo.
Wafanyakazi hao wameiambia BBC kuwa hawajalipwa marupurupu ya waliyoyaita ya hatari kama walivyoahidiwa kwa ajili ya Mwezi Oktoba na Novemba.
Kenema ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Sierra Leone na Mkubwa katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo ambako ugonjwa huo uligunduliwa kwa mara ya kwanza.
Takriban Watu 5000 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu katika nchi za Magharibi mwa Afrika, Guinea,Liberia na Sierra Leone.

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA LINALOMKABILI MFANYABIASHARA MAARUFU DAR LACHUKUA SURA MPYA!


Mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji(mwenye suti), akiwa chini ya ulinzi. Vyanzo vyetu makini kutoka jeshi la polisi zinasema kuwa mali zinazochunguzwa kutokana na tuhuma hizo nzito ni maghorofa, fedha pamoja na magari anayomiliki. “Tuliambiwa kuwa huyu bwana alikuwa akiishi maisha ya hali ya juu, sasa kutokana na tuhumza zake polisi wameanza kuchunguza kila alichonacho ili kujua uhalali wake,” kilisema chanzo. HALI tete, siku chache baada ya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji kukamatwa na kutupwa gerezani kwa tuhuma za kukamatwa na dawa kulevya, sasa mali zake zimeanza kuchunguzwa.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, kuna baadhi ya watoto wa vigogo akiwemo mtoto wa meya mmoja wa zamani (jina tunalihifadhi), jijini Dar es Salaam ambaye anadaiwa kuwa alikuwemo katika mkumbo wa kukamatwa Chonji lakini alitoroka na sasa anasakwa na polisi.Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa alipotafutwa na gazeti hili ili afafanue madai hayo alisema uchunguzi wa mali za wote wanaotuhumiwa kukamtwa na dawa za kulevya ni lazima ufanyike. 
Chonji akiwa chini ya ulinzi mkali na wenzake mahakamani. “Tunachunguza mali zao wote waliokamatwa na tuhuma za dawa za kulevya na siyo kwa Chonji peke yake, inapodhihirika kuwa ni za madawa huwa wanafilisiwa,” alisema Kamanda Nzowa. Chonji na wenzake wanne walikamatwa usiku wa manane Oktoba 21, mwaka huu nyumbani kwake Magomeni Mtaa wa Kondoa jijini Dar na inadaiwa walikuwa na mzigo wa unga uliokuwa ukifungwa katika vifurushi vidovidogo pia anadaiwa kukutwa na sare za jeshi (JWTZ) na bastola

MUOKOE MTANZANIA 15456 BBA MPIGIE KURA.





PIKA KURA KUMTOA IDRISA  KATIKA DANGER ZONE BBA 15456 MTANDAO WOWOTE.

Jumatatu, 24 Novemba 2014

MAGAZETI YA LEO

 http://rashidijuma.blogspot.com/2014/11/peruzi-magazeti-yote-ya-tanzania-ya-leo_25.html

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

MAREKANI: WAZIRI WA ULINZI CHUCK HAGEL AJIUZULU

Barack obama amekubali Jumatatu Novemba 24 ombi la kujiuzulu kwa waziri wake wa ulinzi, Chuk Hagel.
Barack obama amekubali Jumatatu Novemba 24 ombi la kujiuzulu kwa waziri wake wa ulinzi, Chuk Hagel.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel, amewasilisha barua yake ya kujiuzulu Jumatatu Novemba kwenye Ikulu ya Washington. Kujiuzulu huko kumetangazwa na Chuck Hagel wakati wa mkutano na vyombo vya habari, mkutano ambao umehudhuriwa na barack Obama.
Kulingana na kauli ya Barack Obama, Chuk Hagel ndiye ametaka mwenyewe kutamatisha muhula wake kwenye wadhifa aliyokua akishikilia. Kati ya wawili hao hakuna aliyetoa maelezo zaidi kuhusu uamzi huo wa kujiuzulu. Lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, waziri wa ulinzi alikua alipewa shinikizo.
Gazeti la New York Times limebaini kwamba kujiuzulu kwa Chuk Hagel kunahusiana na hali ya kutoelewana iliyojitokeza katika vita vinavyoendeshwa na Marekani dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Iraq na Syria.
Inasadikiwa kuwa Ikulu ya washington huenda ilikua ikitathmini mkakati wake dhidi ya wanajihadi na ilikua inahitaji mkakati huo uanze kutekelezwa na waziri mpya wa ulinzi. Chuck Hagel awali alikuwa na wajibu wa kusimamia uondoaji wa majeshi kutoka Iraq na Afghanistan, wala si kusimamia operesheni ya kijeshi.
Washirika wa karibu wa Barack Obama wamekanusha hoja ya kujiuzulu kutokana na kushinikizwa. " Hakuna tofauti ya maoni ambayo imesababisha Chuk hagel anachukua umazi huo wa kujiuzulu", maafisa wa Ikulu ya Washington wamesema. Maafisa hao wamebaini kwamba mazungumzo ya kujiuzulu kwa Chuk Hagel yalianza wiki mbili zilizopita.
Waziri wa Ulinzi ataendelea kushikilia wadhifa huo hadi atakapopatikana mrithi wake. Majina kadhaa tayari yameanza kutajwa, ikiwa ni pamoja na Michèle Fournoy, aliyekuwa naibu waziri wa ulinzi.

MAHARUSI WAOANA NDANI YA BWAWA LA MAJI

Maharusi wawili walifanya harusi yao katika bwawa lenye lita milioni 1.5 za maji ya bahari .
Bwawa hilo hutumiwa kutoa mafunzo ya kupiga mbizi katika kituo cha Fort William.
Bi Dorota Bankowska mpiga mbizi mzoefu aliolewa na mpenzi wake ambaye ni mwalimu James Abbot nyumbani kwao mjini Plock , Poland mwezi jana lakini akataka sana kufanya jambo la kipekee wanakoishi kama ishara ya kusherehekea harusi yao.

Jumamosi, 22 Novemba 2014

Zaidi 28 wauwawa na wanamgambo Kenya

Wanamgambo wa al-shabaab wanaaminika kutekeleza mauaji hayo.
Polisi nchini Kenya wanasema kuwa wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Al Shabaab wamewauwa kwa kuwapiga risasi zaidi ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja karibu na mpaka wa Somalia.
Maafisa wa ngazi ya juu wamesema kuwa basi hilo lilitekwanyara katika Jimbo la Mandera wakati likiwa njiani kuelekea katika mji mkuu Nairobi.
Watu wasiokuwa waislamu wanasemakana kutengwa na abiria wengine na kisha kupigwa risasi.
Kundi la al-Shabab nchini Somalia limetekeleza mashambulizi kadhaa nchini Kenya tangu mwaka 2011.
Huo ndio mwaka ambapo Kenya iliwatuma wanajeshi wake nchini Somalia kupigana na kundi hilo la waislamu wenye itikadi kali.
Mji wa Mandera katika eneo la Kaskazini mashariki ndio ulioathirika pakubwa. Baada ya shambulio hilo la mapema jumamosi maafisa katika eneo hilo wamenukuliwa na vyombo vya habari nchini kenya wakisema kuwa serikali ilikataa kuitikia ombi lao la kutaka usalama kudumishwa zaidi.
Afisa mmoja ameliambia gazeti la Daily Nation kwamba wavamizi hao waliwataka abiria kusoma aya katika Koran kabla ya kuwaangamiza walioshindwa kufanya hivyo.

JAMAA ALIYEMTWANGA MKEWE TALAKA SIKU YA HARUSI




Jamaa mmoja kutoka nchini Saudi Arabia amempa talaka mkewe siku ya harusi baada ya kumuona uso wake kwa mara ya kwanza. Maharusi hao kutoka mji wa Saudia,Medinah walikubaliana kuoana pamoja na kujua kabisa hawajawahi kuonana sura zao,swala ambalo ni utamaduni mkubwa wa mataifa ya kiarabu.
Lakini wakati mwanamke huyo alipofungua kitambaa cheupe kilichopo katika shela alichokuwa amejifunika uso na kutabasamu katika kamera,mumewe alishtuka na kuondoka wa ghafla.
Mwanamume huyo alianguka na kuzirai huku wageni waalikwa wakijaribu kuingilia kati ili kutatua kilichokuwa kikiendelea. Hata hivyo Bwana harusi alisema kuwa hakuweza kumwona bi harusi kabla ya harusi yao.
'' Si wewe msichana niliyetaka kuoa,si wewe kamwe niliyedhani '' kwa hivyo nakupa talaka''alisema bwana harusi.
Na alipompa talaka bi harusi naye alianguka na kuzirai na kuifanya harusi hiyo kuwa usiku wa majonzi.

Ujue Mmea wa Mlonge na faida zake kwa binadamu(Moringa Tree)



1. Karibu kila sehemu ya mti wa Moringa inatumika au inalika kama chakula. Majani ndio sehemu kuu ya mti wa Moringa, unaweza kuyala yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa kama mboga yoyote ya majani, na pia unaweza ukayakausha na kuyahifadhi kama unga-unga kwa miezi mingi huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi. 

Pia majani yanaweza kutumika kama lishe bora ya mifugo.

Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa majani ya Moringa ni chanzo kikubwa cha virutubishi vingi sana. Virutubishi hivi ni pamoja na;

Vitamini C - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Kiwango chake katikamajani ya Moringa ni zaidi ya mara saba ya ile inayopatikana kutoka kwenye machungwa.

Calcium (madini chuma) - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha pamoja na kujenga mifupa na meno mwilini. Kiwango chake katika majani ya Moringa nimara nne zaidi ya yale yanayopatikana kutoka kwenye maziwa.

Protini - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga mwili na kuimarisha ngozi. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara mbili zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye maziwa.

Vitamini A - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha macho na kuongeza uwezo wa kuona. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara nne zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye Karoti.

Potassium - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga na kuupatia mwili nguvu. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara tatu zaidi ya ile ipatikanayo kutoka kwenye ndizi. Maua ya Moringa yamejaliwa madini chuma (calcium) na Potassium kwa wingi na yanaweza kuchemshwa au kupikwa na kuliwa kama mboga. 

2. Mboga
Majani ya Moringa huliwa kama mboga nyingine za majani kwa mfano mchicha. Majani yanaweza kuvunwa wakati wa kiangazi ambapo mboga nyingine hazipatikani. Pia matunda mateke ya Moringa huweza kutumika kama mboga, hutayariswa kama maharage mabichi (machanga). Matunda yalikomaa hutoa mbegu ambazo zinaweza kutumika kama njegere au kukaangwa kama karanga.

3. Mafuta
Mafuta kutoka kwenye mbegu za mti wa Moringa huweza kutumika katika kupikia na kuwasha katika nyumba. Pia hutumika sana kwenye viwanda katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo. Mafuta hukamuliwa kutoka kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa.

4. Lishe ya Mifugo
Majani ya Moringa huliwa na ng’ombe, mbuzi, kondoo, sungura na kuku. Mbegu huliwa na kuku pamoja na wanyama wengine kwenye jamii ya ndege.

5. Pambo la nyumba
Mti wa Moringa hupandwa kwa wingi kwenye bustani kama ua au mti wa kivuli na hutumika katika upambaji. Pia miti ya moringa ikipandwa karibu karibu inaweza kutumika kama fensi.

6. Chanzo cha kipato
Mti wa Moringa ukitumiwa vizuri ni chanzo kizuri cha kipato. Mfano ni uuzaji wa miche ya mti wa moringa na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na moringa.

7. Tiba mbadala 
Moringa ni mti muhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali.


Majani



  • Majani mabichi ya Moringa ni mazuri kwa kina mama wajawazito na wenye kunyonyesha, huongeza wingi wa maziwa na hushauriwa kwa kutibu Anaemia.
  • Juisi ya majani ya Moringa hutumika kusafisha tumbo na hutibu magonjwa ya zinaa. Juisi ikichanganywa na asali inatibu kuharisha.
  • Pia juisi ina uwezo wa kusawazisha presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye
  • kisukari.
  • Majani pia huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.



Mbegu


  • Mbegu za mti wa Moringa ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi.
  • Pia mbegu hutuminka katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa baada ya kuchemsha.



Magome


  • Magome ya mti wa Moringa hupondwa na kuwa rojorojo kisha hutumika kutibu majipu pia hupakwa ili kupunguza maumivu yatokanayo na kung’atwa na wadudu kama nyoka na nge.



Matumizi mengineyo
Miti ya Moringa ikipandwa shambani huweza kuwa msaada kwa mimea ipandayo kama vile maharage. Pia Moringa ikipandwa bustanini husaidia kupunguza joto la moja kwa moja kufikia mimea kama vile mboga mboga na kupunguza uwezekano wa mboga kusinyaa au kukauka. Mti wa Moringa unaota katika mazingira yote, kwenye ukame na meneo yenye maji. Angalizo huchukuliwa kuhakikisha kuwa maji hayatuami kwenye mti kwasababu maji huweza kusababisha ugonjwa na kufanya mizizi ioze. Karibu aina zote za udongo zinafaa kwa mti wa Moringa. Mbegu, kipande cha tawi na hata mzizi vinaweza kutumika kuotesha mti wa moringa.


Namna ya kupanda mti wa Moringa

I. Mbegu
Mbegu iliyokomaa ya mti wa Moringa hulowekwa siku moja kabla ya kuoteshwa, kama maji sio tatizo mbegu inaweza kupandwa moja kwa moja kwenye udongo baada ya kuchimba shimo, weka maji na kisha changanya udongo na samadi angalau kilo tano kabla ya kupanda mbegu halafu endelea kumwagilia katika miezi ya mwanzo. Baada ya angalau siku kumi na tano mbegu inatakiwa iwe imeshachipua. Pia unaweza kuotesha mbegu za Moringa katika vifuko kwenye kitalu kisha kuhamishia shambani baada ya kuota.

II. Kipande cha tawi
Vipande vya tawi lililo komaa huweza kutumika katika kupanda mti wa Moringa, hivi hupandwa eidha moja kwa moja shambani au kwenye vifuko katika kitalu. Kama ukipandwa moja kwa moja angalau robo moja ya tawi inatakiwa ipandwe kwenye udongo, usimwagilie maji mengi sana kwani inaweza kusababisha kuoza.
 
 
Blogger Templates