Mabingwa wa kombe la mataifa ya Afrika, watafanya kila wawezalo leo usiku kujitafutia nafasi katika fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika. Michuano ya leo ni ya awamu ya mwisho ya kufuzu.
Tayari nchi kumi zimefuzu kwa awamu ya fainali kwa michuno itakayochezwa tarehe 17 Januari hadi 8 Februari mwaka 2015. Mataifa mengine matanao yatajiunga nao kama moja ya timu mbili katika makundi huku tyimu moja ikipata nafasi bora zaidi ya tatu.
Juhudi za Nigeria kupata nafasi hiyo zimekumbwa na changamoto uwanjani na nje ya uwanja, hali ambayo huenda ikaathiri nafasi yao ya kutetea ubingwa wao mwaka ujao.
Lakini itaingia katika mechi ya mwisho dhidi ya Afrika Kusini ambayo tayari imefuzu. Nigeria walikwenda sare ya mabao mawili dhidi ya DRC katika mechi iliyochezwa Jumamosi.
''Haikua mechi rahisi dhidi ya DRC, lakini bahati ilikuwa upande wetu. Ilikuwa hatua kubwa kwetu,'' alisema kocha Keshi ambaye hatamchezesha Hope Akpan ambaye alipata jeraha la bega.
Afrika Kusini hawajashindwa kabisa katika mechi zao tano za kufuzu chini ya kocha Ephraim 'Shakes' Mashaba.
Lakini mkuu huyo wa Bafana Bafana anafahamu vyema kinachomsubiri mjini humo.
Congo ambao wako katika nafasi ya tatu ambao walicheza kwa mara ya mwisho miaka 14 iliyopita, watafuzu kama timu iliyo katika nafasi nzuri zaidi ya tatu ikiwa itashinda Sudan.
Guinea iliicharaza Togo mabao 4-1 wikendi iliyopita, na sasa lazima waishinde Uganda kwa zaidi ya mabao 2-0 katika mechi yao ya mwisho nyumbani ili wajikatie tiketi ya fainali.
Mechi hiyo itachezwa nchini Morocco kwa sababu ya hofu ya Ebola nchini Guinea.
Uganda na Guinea zina alama saba lakini Uganda iko mbele kwa jumla ya alama baada ya kuicharaza Guinea mabao mawili kwa nunge mwezi Septemba.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliwapongeza wachezaji wa timu ya taifa kwa ufanisi wao.
"msiwe na wasiwasi mmefurahisha nchi nzima, kwa hivyo ni vyema mkifuzu ili muweke historia, '' alisema rais Museveni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni