Dr. Ralph Meyering na Profesa Emeritus wa chuo kikuu cha Illinois huko Marekani wanasema inaonekana wanawake hutazama tendo la ndoa nje ya ndoa zao kama jambo tofauti na lile wanalofanya na waume zao.
Kwao kUtoka nje sio kufuata tendo la ndoa hasa. Ni vyema hata hivyo kabla sijazitaja baadhi ya sababu nikasema kwamba hatupaswi kuzichukulia sababu hizo kama msahafu , hapana. Binadamu hubadilika kila siku na suala la hisia na uamuzi wa binadamu nalo limejaa utata pia.

tu mmoja anaweza kutoka nje ya ndoa kwa sababu ambayo mwingine wala asingehisi kuwepo kwake lakini pia zile sababu ambazo zimebainishwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni chanzo cha wanandoa kutoka nje zinaweza zisiwe ndizo hizo ambazo zimemfanya mwanandoa fulani kutoka nje.

Sababu zenyewe ni hizi hapa:

1. Kutafuta kusikilizwa- kuna idadi kubwa a wanawake ambao hutoka nje ya ndoa zao kutafuta kuziba pengo la kihisia. Kwa kawaida mwanamke hupenda kuona mwanaume akimjali, akimsikiliza na kuwa karibu naye kihisia, na kama jambo hili halitimizwi na mumewe, basi atatafuta mtu wa kuziba pengo hilo huko nje. Kuna wakati unaweza kumsikia mwanaume akilalamika, “nimeamua kuachana na mwanamke yule. Nilikuwa nampa kila kitu lakini bado akawa anatoka nje ya ndoa.” Ndio inawezekana alikuwa anampa mkewe kila kitu, lakini alisahau kuwa mwanamke ni zaidi ya mali.

2. Kutafuta kukamilishwa- kuna wanawake hudhani kwamba umri wao umekuwa mkubwa na hawana thamani tena, yaani hawawezi kupendwa. Hofu ya kwamba wamezeeka au hawapendeki inaweza kuwafanya kuwa wepesi na kukubali kutoka nje ya ndoa ili kujithibitishia kwamba hawajachuja au kupoteza thamani zao. Sababu hii pia huwaangukia pia wale wanawake ambao hawajaolewa lakini wanatembea na vijana wadogo waliowazidi umri.

3. Kulipa kisasi- Ingawa sio wanawake wengi wanaolipa visasi kufuatia waume au wapenzi wao kuwa na uhusiano nje, bado kuna idadi a kutosha ya wanawake wanaofanya hivyo. Mara nyingi hutokea kwa wale ambao walikuwa na hisia ya kutoka nje lakini walikuwa anazikandamiza hisia hizo, hivyo inapotokea kupata sababu, ni rahisi sana kwao kutoka nje.


4. Kuwa huru katika mapenzi- kuna wakati tendo la ndoa kwa wandoa au wapenzi linakuwa ni tendo la mwanaume zaidi. Yeye ndiye anayeamua lifanyike vipi na wakati gani. 
Mwanamke anakuwa hana kauli kabisa kwenye jambo hili. Mwanamke anayeishi kwenye ndoa au uhusiano wa aina hii hufikia mahali tendo la ndoa na mumewe au mpenzi wake linakuwa ni aina ya utumwa. Ni rahisi sana kwa manamke anayeishi kwenye husiano wa aina hii kutoka nje ya ndoa ili kutafuta ule uhuru ambao haupati kwa mumewe.


5. Matatizo ya kipato- hili linafahamika kwa wengi kati yetu. Mwanamke anatoka nje ya ndoa yake ili amudu kujikimu kutokana na ugumu wa hali ya kimapato. Kuna wanawake ambao wametelekezwa au waume waume zao hawana kipato. Baada ya kuhangaika sana hulazimika kuutoa mwili wake kwa walichonacho ili mkupata fedha au kazi. Maofisini kuna waawake wengi ambao wanaishi kwenye kazi zao kwa kutoa miili yao kwa mabosi au wamiliki wa ofisi hizo kwa sababu wanataka kuendelea kuwa kazini.

6. Kutoridhishwa katika tendo- Kabla ya miaka ya Sabini tafiti zinaoneshwa kwamba tendo la ndoa halikuwa linahesabika kwa ridhiko la mwili bali zaidi lilikuwa ni ishara ya kupendana na kutafuta watoto. Lakini leo hii tendo la ndoa limekuwa ni burudani, lenyewe kama lilivyo. Kwa hiyo mpenzi anapokuwa na udhaifu hata kidogo, sio ajabu mwenzake kuhisi kwamba anakosa jambo kubwa na muhimu kuliko hata uhusiano wenyewe. Katika hali kama hiyo anaweza kuanza kutafuta mtu ambaye anaamini atamfanya ahisi ridhiko. TV na mikanda michafu ya video imeongeza uongo kuhusu ridhiko la tendo la ndoa, kiasi kwamba yule ambaye mpenzi wake ana udhaifu huamini kwamba anakosa kikubwa kama kinavyoonekana kwenye TV na mikanda michafu ya video.

7. Tamaa ya kipato- Inashauriwa kwamba mwanaume anapokwenda kuoa inabidi aende kama yeye, yaani akionesha na kusema kuhusu alivyo, bila kuongeza chumvi. Wanashauri pia kwamba mwanaume anapokwenda kuoa akague namna msichana alivyolelewa yaani aina ya malezi ya wazazi wa mwanamke. Kuna wanawake ambao hawako tayari kukosa kile wanachokitaka maishani. Wanapokikosa wanakuwa tayari kufanya lolote, ikiwa ni pamoa na kuuza miili yao.

Kwenye utafiti wake alioufanya, Dk. Lynn Atwater anaonesha kwamba nusu ya wanawake wanaotoka nje ya ndoa zao wanakuwa wamewajua hawara zao miezi kadhaa kabla hawajafanya nao tendo la ndoa.
Nusu waliobaki wanakuwa wamewafahamu angalau kwa katika kipindi cha mwaka mmoja kabla hajaama kufanya nao mapenzi. Kabla mwanamke hajakubali kufanya nmapenzi na hawara huwa ameshafanya uamuzi huo sio chini ya mwezi mmoja kabla. 

Kwa hiyo unapokuta umehangaika kumpata mke wa mtu kwa muda mrefu, unapokuja kumpata, basi jua kwamba Alisha kukubalia mwezi mmoja au zaidi kabla ya siku hiyo.

Mara nyingi mwanamke akikubali, kabla hajamjulisha rasmi hawara yake kwamba yuko tayari, ni lazima pia apate ushauri au azungumze na rafiki yake wa karibu sana. Unapofanya mapenzi na mke wa mtu ambaye umemhangaikia kwa muda mrefu, usidhani hiyo ni siri yenu, kuna mwingine amejulishwa. 

Ni wanawake wachache sana wanaobaki na siri hiyo wenyewe.