Social Icons

Jumapili, 11 Januari 2015

OZIL ANAREJEA KAZINI LEO ARSENAL IKIPAMBANA NA WABISHI STOKE.


Kiungo Mesut Ozil atarejea uwanjani kesho wakati Arsenal inakipiga dhidi ya Stoke City.


Ozil inarejea Ligi Kuu England baada ya kukaa nje miezi mitatu kutokana na maumivu ya goti.

Kocha Arsene Wenger amesema Ozil amekuwa akifanya mazoezi na wenzake na sasa yuko fiti, hata hivyo inaonekana ataanzia benchi.

Mjerumani huyo aliyejiunga na Arsenal akitokea Madrid aliumia katika mechi dhidi ya Chelsea, Oktoba mwaka jana.

Ozil ndiye mchezaji ghali zaidi Arsenal iliyompata kwa kitita cha pauni milioni 42.5.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates