Social Icons

Alhamisi, 30 Oktoba 2014

Bunge lachomwa moto pamoja na nyumba za wabunge, rais agoma kuachia madaraka

Burkina FA
Mbali na maafa makubwa yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na majengo ya bunge kuchomwa moto pamoja na nyumba za wabunge, rais aliye madarakani amegoma kuachia madaraka yake.

Blaise Compaore rais wa Burkina Faso aliyekaa madarakani kwa miaka 27 anatajwa kuwa mmoja wa marais waliokaa madarakani kwa kipindi kirefu zaidi na bado anasisitiza kuwa ana miezi 12 zaidi ya kuendelea kuwepo madarakani kabla ya kukabidhi madaraka kwa rais ajaye.
Ban Ki-moon anatarajiwa kuwasili nchini siku ya leo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya machafuko hayo.
Chanzo cha machafuko hayo kinatajwa kuwa ni kitendo cha bunge kutaka kufanya mabadiliko ya katiba ambayo yangemfanya Blaise Compaore kubakia madarakani kwa kipindi kingine zaidi.
Burkina FBurkina FAS
Burkina-Faso-600x337
Taarifa zinasema jeshi limelazimika kuongoza nchi hiyo ili kurejesha utulivu.

HII NDIO IBARA 28 ILIYONYOFOLEWA NA BUNGE LA KATIBA

Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba


Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iliyowasilishwa bungeni juzi, imeondoa Ibara 28 zikiwamo zinazowataka viongozi wa umma kutopokea zawadi kwa manufaa yao binafsi wala kufungua akaunti ya benki nje ya nchi pasipo sababu maalumu, Mwananchi limebaini.
Ibara ya 15 iliyokuwamo katika Rasimu ya Warioba ilisema: “Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, zawadi hiyo itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ilitaka Bunge kutunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano. Mbali na ibara hiyo, pia Ibara ya 16 iliyohusu ufunguaji akaunti nje ya nchi, imeondolewa.
Ibara nyingine zilizoondolewa ni pamoja na ya 17 iliyopendekeza uwazi wa mali ikimtaka kiongozi wa umma kutangaza thamani ya mali na madeni yake mara tu baada ya kupata uongozi.
Pia Ibara ya 129 iliyokuwa inawaruhusu wananchi kumvua madaraka mbunge ambaye atashindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapigakura wake au ataacha kuishi au kuhamisha makazi yake kutoka eneo la jimbo la uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi imeondolewa.
Ibara 28 zilizoondolewa
15. (1) Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ataiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi kupitia kwa katibu mkuu wa wizara au kiongozi wa taasisi ya Serikali inayohusika, akiainisha:
(a) aina ya zawadi; (b) thamani ya zawadi; (c) sababu ya kupewa zawadi; na (d) mtu au mamlaka iliyotoa zawadi hiyo.
(2) Neno “zawadi” kama lilivyotumika katika ibara hii linajumuisha kitu chochote chenye thamani atakachopewa kiongozi wa umma katika utekelezaji wa shughuli za umma.
(3) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano.
16. Kiongozi wa umma-
(a) Hatafungua au kumiliki akaunti ya benki nje ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kwa namna ambayo sheria za nchi zinaruhusu; na (b) hataomba au kupokea mkopo au faida yoyote kwa namna au mazingira ambayo yanashusha hadhi au heshima ya utumishi wa umma.
17.-(1) Kiongozi wa umma atalazimika kutangaza na kuwasilisha, ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi, mali na thamani yake na madeni yake katika Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya(1), Kiongozi wa umma atalazimika kutangaza na kuwasilisha taarifa ya mali na madeni: (a)yake binafsi; (b) ya mwenza wake wa ndoa; na(c) ya watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane, mara moja kila mwaka kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.
(3) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine: (a) ngazi au orodha ya viongozi wa umma wanaopaswa kutangaza mali na madeni yao; na (b) utaratibu wa kuwasilisha taarifa ya mali na madeni kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji kwa mujibu wa Katiba hii.
18.-(1) Kiongozi wa umma hatashiriki katika kufanya uamuzi wa jambo au shughuli yoyote ambayo ana masilahi nayo yeye binafsi, mwenza wake, mtoto wake, jamaa yake, rafiki au mtu yeyote wa karibu.
(2) Kiongozi wa umma hatazungumzia kitu chochote katika Baraza la Mawaziri, Bunge, Kamati au chombo kingine chochote rasmi ambacho ana masilahi nacho ya moja kwa moja au vinginevyo, isipokuwa tu kama atatoa taarifa ya mgongano huo wa masilahi katika chombo hicho.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa kiongozi wa umma kushiriki katika uamuzi unaohusu kuongeza au kuboresha masilahi kwa namna yoyote ile yanayohusu wadhifa alionao na endapo atashiriki, basi masharti hayo mapya yataanza kutumika kwa kiongozi wa umma atakayekuja baada ya kiongozi husika kuondoka au kumaliza muda wa kukaa katika nafasi ya madaraka iliyompatia fursa ya kushiriki katika kuamua masilahi husika.
(4) Masharti ya ibara ndogo ya (3), hayatamhusu kiongozi wa umma ambaye kutokana na asili ya nafasi ya madaraka au aina ya kazi zake anapaswa kushiriki katika upangaji wa mishahara au maslahi mengine ya watumishi wa umma.
(5) Kiongozi wa umma hataruhusiwa kushika nafasi za madaraka zaidi ya moja au kutumikia mihimili ya dola zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.
19. Kiongozi wa umma hataruhusiwa kutumia au kuruhusu kutumika kwa mali yoyote ya umma, zikiwemo zilizokodishwa kwa Serikali, kwa madhumuni ya kujipatia yeye binafsi au kumpatia mtu mwingine manufaa yoyote.
20.-(1) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine:
(a) utaratibu wa utwaaji wa mali za viongozi wa umma zilizopatikana kwa kukiuka sheria;
(b) utaratibu wa kumwajibisha kiongozi wa umma aliyekiuka maadili na Miiko ya Uongozi; na
(c) uanzishaji wa mitalaa inayohusu Katiba, maadili na uraia, shuleni na vyuoni.
(2) Masharti yaliyoainishwa katika sehemu hii ya Sura ya Tatu yatatumika pia kwa watumishi wa umma baada ya kufanyiwa marekebisho stahiki.
63. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika Ibara ya 61, Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka juu ya mambo ya Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Katiba hii. Nchi Washirika.
64.-(1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Nchi Washirika ni Tanganyika na Zanzibar.
(2) Serikali ya Tanganyika itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanganyika.
(3) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Zanzibar.
(4) Nchi Washirika zitatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.
(5) Nchi Washirika zitakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano na zitatekeleza majukumu yao kwa mambo yote yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Nchi Washirika kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na Katiba za Nchi Washirika.
67.-(1) Kila Nchi Mshirika itateua Waziri Mkaazi atakayeratibu na kusimamia mahusiano baina ya Serikali za Nchi Washirika na kati ya Serikali ya Nchi Mshirika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Mawaziri Wakaazi watakuwa na ofisi zao na watafanya kazi wakiwa Makao Makuu ya Serikali ya Muungano.
(3) Pamoja na majukumu mengine watakayopangiwa na Serikali za Nchi Washirika, Mawaziri Wakaazi watakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) kushughulikia mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu ushirikiano au uhusiano wa kimataifa; na
(b) kuwa kiungo baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika na baina ya Serikali za Nchi Washirika.
68.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itapata mamlaka yake kutoka kwa wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na kusimamiwa na chombo kitakachopewa mamlaka na Katiba hii, na vilevile, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitapata mamlaka kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na kusimamiwa na vyombo vitakavyopewa mamlaka chini ya Katiba zao.
(2) Serikali za Nchi Washirika, katika kutekeleza mamlaka zao, zitawajibika kustawisha mamlaka ya wananchi kwa kugatua madaraka kwa serikali za mitaa zitakazoanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika au Katiba ya Zanzibar, kama itakavyokuwa.
99.-(1) Kutakuwa na Waziri Mwandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano atakayeteuliwa na Rais na kuthibitishwa na Bunge.
(2) Waziri Mwandamizi kabla ya kushika madaraka yake, ataapa mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kama itakavyoelezwa na sheria za nchi.
(3) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Waziri Mwandamizi endapo atakuwa na sifa zilizoainishwa katika Ibara ya 101.
(4) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mwandamizi atashika madaraka ya Waziri Mwandamizi hadi:
(c) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika madaraka ya urais; au
(d) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au
(e) siku atakapojiuzulu; au
(f) siku ambapo Rais atakapomteua mtu mwingine kushika madaraka ya Waziri Mwandamizi.
100.-(1) Waziri Mwandamizi atakuwa na madaraka ya udhibiti na usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za Serikali za siku hadi siku.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mwandamizi atatekeleza majukumu yote atakayoelekezwa na Rais na katika utekelezaji wa majukumu yake atawajibika kwa Rais.
103.-(1) Mawaziri na Naibu Mawaziri hawatakuwa na haki ya kuhudhuria vikao vya Bunge isipokuwa tu:
(a) endapo kutakuwa na hoja mahususi ambayo Bunge linahitaji ufafanuzi kwa waziri husika; au
(b) endapo Serikali au waziri ataomba na kuruhusiwa kuwasilisha au kuitolea ufafanuzi hoja yoyote Bungeni.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), waziri atakayeruhusiwa kuhudhuria kikao cha Bunge anaweza kulihutubia Bunge.
(3) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya uamuzi juu ya sera za Serikali kwa jumla.
(4) Kila waziri atahudhuria vikao vya Kamati za Bunge kila atakapohitajika na kutoa maelezo au ufafanuzi wa suala lolote linalohusu utendaji katika nafasi ya madaraka yake.
(5) Kwa kuzingatia masharti mengine ya jumla ya Katiba hii, mawaziri watatoa maelezo au taarifa ambazo zinahitajika kutolewa bungeni kwa mujibu wa sheria za nchi.
106.-(1) Kutakuwa na Makatibu Wakuu watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi waandamizi katika utumishi wa umma kama watakavyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma.
(2) Kila Katibu Mkuu atakuwa kiongozi na Mtendaji Mkuu wa Wizara ya Serikali aliyopangiwa na Rais na atashika nafasi ya madaraka ya Katibu Mkuu na kutekeleza majukumu yake kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.
(3) Rais anaweza, kwa mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma, kumteua mtumishi mwandamizi katika Utumishi wa Umma kuwa Naibu Katibu Mkuu.
(4) Kila Katibu Mkuu atakuwa mshauri wa mwisho kwa Waziri kwa masuala yote ya utendaji na atatoa ushauri kwa Baraza la Mawaziri katika vikao na kamati zitakazoitishwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri.
(5) Katibu Mkuu au Naibu Katibu Mkuu hatashika madaraka yake hadi awe ameapa mbele ya Rais kiapo cha utii na uaminifu au kiapo kingine chochote kinachohusu utendaji wa kazi zake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
107. Kutakuwa na Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu itakayoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi ambayo itakuwa na majukumu ya kuchambua na kulishauri Baraza la Mawaziri juu ya masuala mbalimbali kabla ya kuwasilishwa na kufanyiwa uamuzi na Baraza hilo na itatekeleza majukumu mengine kama itakavyopangiwa na Baraza la Mawaziri.
112.-(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali itakayoongozwa na Katibu akisaidiwa na Naibu Katibu ambao watateuliwa na Rais.
(2) Mtu atateuliwa kuwa Katibu au Naibu Katibu ikiwa ana sifa zifuatazo:
(a) ni mtumishi mwandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali za Nchi Washirika;
(b) ana shahada kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi; na
(c) ana mwenendo usiotiliwa shaka na jamii.
(3) Katibu na Naibu Katibu watawajibika kwa Tume na watafanya kazi na kutekeleza majukumu ya Sekretarieti.
(4) Uteuzi wa Katibu na Naibu Katibu wa Tume utafanywa kwa kuzingatia msingi kwamba endapo Katibu atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Naibu Katibu atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
120.-(1) Bunge litatumia madaraka yake ya kutunga sheria kwa kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria ambao utawekwa saini na Rais.
(2) Bila kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (3), Muswada wa Sheria unaweza kuandikwa na Serikali, Kamati ya Bunge au kikundi cha Wabunge.
(3) Wakati wa kuandaa Muswada wa Sheria kuhusu jambo lolote la Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kwamba inawashirikisha wananchi kwa ajili ya kupata maoni na mapendekezo juu ya muswada huo.
(4) Muswada wa sheria utahesabiwa kuwa umepitishwa na Bunge iwapo utaungwa mkono kwa kura za wabunge wasiopungua theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Tanganyika na wasiopungua theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Zanzibar.
(5) Bila kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (4), Bunge litatunga Kanuni za Kudumu zitakazoweka utaratibu wa-
(a) kuwasilisha, kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria; na
(b) utekelezaji bora wa masharti ya ibara ndogo ya (3).
129.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, wananchi watakuwa na haki ya kumwondoa mbunge wao madarakani, endapo mbunge atafanya moja wapo au zaidi ya mambo yafuatayo:
(a) kuunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na masilahi ya wapigakura au kinyume na masilahi ya Taifa;
(b) kushindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapigakura wake;
(c) kuacha kuishi au kuhamisha makazi yake kutoka eneo la Jimbo la Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi; au
(d) mambo mengine yatakayoainishwa kwenye sheria ya nchi.
(2) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya kuendesha uchunguzi kwa Mbunge atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa wapigakura wake na utaratibu wa kumwondoa katika ubunge.
146.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, ni marufuku kusema uongo bungeni na kwa sababu hiyo, mbunge anapozungumza ndani ya Bunge ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni la kweli na siyo jambo la kubuni au la kubahatisha.
(2) Mbunge anapokuwa akizungumza bungeni hatahesabika wala kutafsiriwa kuwa anasema uongo iwapo anafanya rejea ya habari kuhusu jambo lililotangazwa au lililoandikwa na vyombo vya habari au nyaraka nyingine yoyote ambayo chanzo chake kinafahamika au kitaelezwa na mbunge huyo.
231. Vyanzo vya mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano vitakuwa:
(a) ushuru wa bidhaa;
(b) mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na taasisi za Muungano;
(c) mchango kutoka kwa nchi washirika;
(d) mikopo kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano; na
(e) mapato mengine.
234. Serikali za nchi washirika zitakuwa na benki zitakazokuwa na jukumu la kutunza akaunti ya fedha za Serikali ya nchi mshirika husika, kusimamia sera za kifedha na benki za biashara katika mamlaka zao.
242.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania itakayokuwa na jukumu la kusimamia masuala yote ya utumishi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu muundo, majukumu na mambo mengine yanayohusu Tume ya Utumishi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
244.-(1) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano litazingatia-
(a) viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu miongoni mwa wafanyakazi wake;
(b) ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu;
(c) kanuni za uwazi na uwajibikaji; na
(d) kukuza uhusiano na jamii.
(2) Jeshi la Polisi, katika kutekeleza majukumu yake, litashirikiana na vyombo vinavyohusika na kupambana na uhalifu vya Nchi Washirika katika kufanya uchunguzi na kushughulikia makosa ya rushwa na ufisadi.
246. Mkuu wa Jeshi la Polisi atatekeleza kazi zake kwa uhuru, bila woga, upendeleo wala chuki na kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria za nchi.
247.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi itakayokuwa na jukumu la kusimamia utumishi wa Jeshi la Polisi.
(2) Katika uajiri wa askari wa Jeshi la Polisi, Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi itazingatia kanuni na misingi ya utumishi iliyoainishwa katika Katiba hii.
(3) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya muundo na utekelezaji wa kazi na majukumu ya Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi.
250.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sura hii, Wakuu wa Nchi Washirika wanaweza kumwagiza kiongozi yeyote wa Jeshi la Polisi au Idara ya Usalama wa Taifa kuchukua hatua yoyote ambayo ni muhimu kwa ajili ya kulinda au kuimarisha usalama wa eneo lolote la Nchi Mshirika husika.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoainisha masharti yanayohusu namna bora ya utekelezaji wa Ibara ndogo ya (1).
253.-(1) Watumishi wafuatao hawatakuwa na haki ya kugombea, kuchaguliwa au kuteuliwa katika nafasi ya kisiasa hadi utakapopita muda wa miaka mitatu tokea kuacha au kustaafu nafasi ya madaraka aliyokuwa akiishikilia:
(a) Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Jaji wa Mahakama ya Juu wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(d) Spika na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(e) Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama;
(f) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(g) Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(h) Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano; na
(i) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mkurugenzi wa Uchaguzi;
(j) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu;
(k) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji;
(l) Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma;
(m) Msajili wa Vyama vya Siasa.
(2) Bunge linaweza kutunga sheria kuhusu aina nyingine ya watumishi wa umma ambao hawataruhusiwa kushika nafasi za madaraka ya kisiasa kwa mujibu wa Ibara hii.

29 WAITWA KIKOSI CHA MABORESHO TAIFA STARS

nooi

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajia kuendelea na awamu ya pili ya maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars) inayojumuisha vijana wenye umri chini ya miaka miaka 23.
Katika awamu hii, Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij ameteua majina ya wachezaji 29 ambao watakuwa wakiingia kambini mara moja kwa mwezi siku ya Jumapili baada ya kuwakilisha timu zao kwenye mechi za ligi.Kikosi hicho cha maboresho kitakuwa kikifanya programu maalumu za mazoezi mpaka siku ya Jumatano na kucheza mechi za kirafiki na timu za ndani au nje ya nchi.Lengo hasa la programu hiyo ni kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji ambao walipatikana katika awamu ya kwanza ya mpango wa maboresho mwanzoni mwa mwaka huu Tukuyu mkoani Mbeya, lakini wamekuwa hawatumiki. Pia kuwandaa vijana ili kujenga timu ya ushindani na imara ya Taifa ya muda mrefu.

TFF ina imani kubwa kuwa programu hii itakuwa na manufaa kwa soka ya Tanzania. Timu hiyo itaingia kambini kwa mara ya kwanza Desemba 9 mwaka huu katika hoteli itakayotangazwa baadaye.
Wachezaji walioteuliwa ni Aishi manula (Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar), Aboubakar Ally (Coastal Union), Miraji Adam (Simba), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Gadiel Mbaga (Azam), Emmanuel Semwanda (African Lyon) na Joram Mgeveke (Simba).
Edward Charles (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kassim Simbaulanga (African Lyon), Pato Ngonyani (Yanga), Adam Salamba (Kahama), Hassan Banda (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hashim Magoma (Stand United), Makarani Ally (Mtibwa Sugar), Said Juma (Yanga) na Said Hamis (Simba).
Aboubakary Ally Mohamed (Zanzibar), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Malombe (Geita Gold), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda SC), Kelvin Friday (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Alfred Masumbakenda (Kahama) na Simon Msuva (Yanga).

NI KWELI HIKI NDICHO KINACHO PELEKEA TBC 1 KUSHIKA NAFASI YA MWISHO KUTAZAMWA.

 

Kwa hali ya kushangaza, kituo cha television cha matangazo cha tbc 1 kati ya vituo vinne maarufu vya matangazo ya habari nchini Tanzania kimeshika nafasi ya mwisho baada ya kufanyiwa utafiti,

Kwa habari za uhakika ni kwamba kituo kilichoongoza kuangaliwa na watazamaji wengi ni ITV kikifuatiwa na Star TV, nafasi ya tatu imeshikwa na Channel 10 na hatimaye TBC1.

Kwa utafiti uliofanya na na TCRA imebainika kuwa ni aibu kama kituo television ambacho ni cha Taifa na ni UMMA kushika mkia nyuma ya vituo binafsi jambo ambalo ni hatari.

Vyanzo vya kuaminika vinadai kuwa TBC1 imefikia hapi baada ya kugundulika inabagua baadhi ya habari ya vyama vya siasa na kutoa habari ya chama kimoja tuu jambo ambalo siyo sahihi katika utashi wa utangazaji na kutofuata uhuru wa kiutangazaji ndani ya uongozi wa shirika la habari la Tanzania, 

Utafiti umeonyesha kuwa ili chombo cha habri kiweze kuangaliwa na watu wote wa vyama vyote ni lazima chombo cha habari kitoe habari bila kubagua vyama vya siasa maana watazamaji wana misimamo tofauti na itikadi tofauti, na kama chombo cha habari kikiamua kutoa habari kwa chama kimoja cha siasa basi ujue hapo watakaoangali hizo taarifa za habari ni hao hao wa chama kimoja.

Watafiti pia walienda mbali zaidi na kukinyoshea vidole kituo cha taifa cha utangazaji kuwa ni chombo cha UMMA na kisipende kubagua baadhi ya taarifa za habari za vyama vya siasa kwa misingi ya kuelekezwa na wanasiasa au viongozi wa nchi maana madhara yake ni wananchi kushindwa kuangalia hicho kituo.

Mwisho wake kitashindwa kufanya biashara na hatimaye kutegemea tuu ruzuku serikalini na hapo ndo nchi itazidi kupata hasara badala ya kukiacha chombo kijiendeshe kwa uhuru. Wametoa mfano kama shirika la habari la Uingereza BBC lingefanya kama TBC inavyofanya basi nayo ingeishia kutazamwa tuu nchini uingereza na tena kwa watu wachache tofauti na ilivyo sasa BBC inatazamwa duniani kote.

Utafiti umeonyesha kuwa hivi vyombo vingine vya habari ITV, Star TV na Channel 10 vimepata watazamaji wengi kwa kuwa havibagui matangazo ya kada tofauti ya vyama vya siasa na hapo ndoo inasababisha waweze kupata watazamaji wa kutosha.

MAGAZETI YA LEO



.

.

.

.

..

.

.

.

.

.

.

.


.

.

.

.


.

.

.

.

.

.

.

Jumatano, 29 Oktoba 2014

HATIMAYE CHIDI BENZI APATA DHAMANA

Chid Benz akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.

HATIMAYE  msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro 'Chid Benz' leo asubuhi amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kesi yake ya kukamatwa na dawa za kulevya.
Msanii huyo, jana alipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka matatu ya kukutwa 


na madawa ya kulevya ambapo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana ya shilingi milioni 1 pamoja na wadhamini wawili wasiokuwana hatia.

Kesi yake itasikilizwa tena Novemba 11 mwaka huu.

KOFI ANNAN: EBOLA NI UGONJWA WA WATU MASKINI NA SIO MATAJIRI=

Mwana Diplomasia kutoka Ghana ambaye pia ni Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN) Kofi Annan amesema ugonjwa wa Ebola ni wa ‘maskini’ na sio matajiri.Annan amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha CNN ambapo amezungumzia sababu kadhaa zinazopelekea mapambano ya dhidi ya Ebola kuchukua muda mrefu huku maelfu ya watu wakipoteza maisha.Katibu Mkuu huyo mstaafu amesema Ebola ni ugonjwa wa maskini kwa kuwa tangu ugundulike ni takribani miaka 40 imepita, ambapo kwa nchi tajiri ingewezekana kufanyika tafiti ambazo zingesaidia kupata ufumbuzi wa tiba ya ugonjwa huo, kitu ambacho nchi maskini za Afrika hazina uwezo wa kuwekeza kwenye tafiti hizo.


Aidha, Annan ameonekana kuvunjwa moyo na jitihada zinazofanywa na mataifa makubwa ikiwemo Marekani kutangaza utaratibu mwisho wa wiki iliyopita wa kuwaweka karantini wauguzi na madaktari waliotoka Afrika Magharibi kwa siku 21, kitu ambacho kinarudisha nyuma ari ya wahudumu hao kujitolea kusaidia wagonjwa kwenye nchi zilizoathirika na Ebola.

Amesema njia pekee ya kuimaliza Ebola ni kufanya jitihada na mapambano ya pamoja katika kuzisaidia nchi za Afrika Magharibi na sio kwingineko, na kuongeza kuwa Afrika inachohitaji ni msaada wa vifaa, madawa na wauguzi ili kupambana na Ebola.

Mpaka sasa Liberia, Guinea na Sierra Leone zimetajwa kuathiriwa zaidi na Ebola,huku takwimu zikionesha zaidi ya watu 4,900 wamefariki na wngine zaidi ya 10,000 kupatwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

Rais wa kwanza mzungu ndani ya Afrika

Guy Scott
Guy Scott ambaye alikuwa makamu wa rais Zambia wakati wa utawala wa Michael Sata ametajwa kushika nafasi ya urais wa nchi hiyo kwa sasa mpaka pale ambapo ataapishwa mara baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.Waziri wa ulinzi Zambia Edgar Lungu amesema maandalizi ya uchaguzi huo yataanza muda wowote ambapo katiba ya nchi hiyo inaagiza kufanyika uchaguzi wa Rais ndani ya siku 90 baada ya kufariki kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo.

Scott ameteuliwa kushika wadhifa huo ambapo hii itakuwa mara ya kwanza kwa rais mzungu kuongoza nchi ya Afrika tangu kuisha kwa kipindi cha ubaguzi wa rangi Afrika Kusini chini ya utawala wa FW de Klerk.
Kulikuwa na utata uliotokana na katiba ya Zambia kumruhusu Scott kushika wadhifa huo kwa sababu wazazi wake wanatokea Scottland, huku katiba hiyo ikitaja rais wa nchi hiyo ni lazima awe Mzambia kamili kwa maana ya kwamba wazazi wake wote wawili wanapaswa kuwa wamezaliwa nchini humo.

Jumanne, 28 Oktoba 2014

JWTZ WATEGUA BOMU LILOTEGWA KATIKA ENEO LA KITUO CHA KURUSHIA MATANGAZO CHA TBC SONGEA‏

Bomu lililotengenezwa kienyeji  kama linavoonekana katika picha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa mtaaram wa mabomu ambaye ni kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kabla ya kulitegua bomu hili.


Hili ni eneo la tukio ambalo limezungushiwa mkanda huu wa pilisi uliandikwa hairuhusiwi kupita eneo hili,Lakini chini ya huo mti kama inavoonekana katika picha kukiwa na udongo umetifuliwa ndipo mahara ambapo lilitegwa bomu hili la kutengenezwa kienyeji pia hapo ndipo huwa wanakaa askari wa Usalama barabarani kwa kujikinga na jua ama kupumzika pindi wanapokuwa kazini
Bomu lililotengenezwa kienyeji


Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji.
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiwa anaonyesha umahili wake alionao aweze kulitegua bila kuleta madhara yoyote yale katika jamii(Picha na demasho.com)
-------------------------
 Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania(JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia matangazo kilichopo mshangano cha shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya saa moja jioni.

Bomu hili linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji nawatu wasiojulikana lilitegwa hatua  zinazokadiliwa thelathini kutoka kitika kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao za kila siku.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwamujibu wa wataalamu wa milipuko kutoka jeshi la Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili linaonekakana limetengenezwa kienyeji.
ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji askari polisi watatu  wakiwa katika doria katika kata ya misufini manispaa ya songea.

Msikhela amesema Jeshi la polisi linafanya jitihada za kuwapata watu hawa wanaohusika na mtandao huu wa utegaji wa mabomu na ulipuaji, Aidha ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa Jeshi la Polisi ili liweze kuwabaini watu wanaousika na matukio ya namana hii.

Na hii ni mara ya pili katika manispaa ya songea kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe Oktoba 16 mwaka huu askari watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,  walijeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo lilisadikiwa kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe mjini songea mkoani Ruvuma.

Askari hao walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika doria ambao ni WP Felista Abel, PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na mtandao huu wa demasho  kwa njia ya simu amesikitishwa na kitendo hicho cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha amani iliyopo katika mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata walewote wanaohusika na vitendo hivi.

 
 
Blogger Templates