Hivi karibu gazeti la The Sun liliripoti juu ya tuhuma za kumhusu kiungo wa timu ya Newcastle Cheick Tiote na familia yake.
Tiote, ambaye anavuna kiasi cha paundi £45,000 kwa wiki kupitia klabu yake ya Newcastle, ameripotiwa kufunga ndoa ya kimila na Laeticia Doukrou mwezi uliopita, japokuwa tayari ameshaoa mke mwingine aitwaye – Madah mwenye umri wa miaka 25.
Kiungo huyo mwenye miaka 28, kwa sasa anaishi na Madah pamoja na watoto wao wawili katika jumba lao lenye thamani ya £1.5million Ponteland karibu na Newcastle, pia Tiote ana mtoto mwingine nje ya ndoa zake na mwanamke wa nje aitwaye Nikki Mpofu.
Wakala wa mchezaji huyo Jean Musampa amethibitisha kuhusu mchezaji kuoa mara ya pili, alisema: ‘Ninachoweza kusema ni kwamba ni kweli ameoa na hiyo ni ndoa yake ya pili.
‘Hiki ni kitu cha kawaida, Tiote ni muislam, sheria za kidini zinamruhusu kuoa hadi wake wanne, hivyo hakuna kibaya alichofanya.This is nothing unusual. He is a Muslim.’
Tiote pia anaripotiwa kuwaambai marafiki zake kwamba haoni shida kuwa na wanawake wengi, na hata nyumbani kwao Ivory Coast ameshwakuwa na mahusiano na wanawake wengi. Gazeti la The Sun limeripoti.
Gazeti hilo pia limeripoti kwamba mahusiano kati ya Tiote na ‘hawara’ yake Nikki Mpofu yamefikia ukingoni baada ya miaka mitatu baada ya mwanamke huyo raia wa Zimbabwe kuchoshwa na ahadi za uongo za kuolewa na mchezaji huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni