Mwalimu mmoja raia wa Uingereza ambaye alitekwa nyara nchini Libya mwezi Mei mwaka huu ameachiliwa huru
Wizara ya masuala ya kigeni nchini Uingereza imethibitisha kuwa David Bolam ambaye alikuwa akifanya kazi na shule moja ya kimataifa kwenye mji ulio mashariki wa Benghazi yuko salama salmin.
Haijulikani ni nani aliyemteka nyara,lakini inaaminika kuwa kundi moja la kiislamu.
Vilevile inaamimika kuwa kuwachiliwa kwake kulitekelezwa na makundi ya wansiasa wa eneo hilo na kwamba kikombozi kililipwa ili kumwachilia huru,ijapokuwa haijulikani ni pesa ngapi.
Mwandishi wa BBC ameambiwa kuwa shule aliyokuwa akiifanyia kazi ilitakiwa kulipa fidia.
Bolam tayari asharudi nchini Uingereza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni