Baada ya Ushindi wa Redds Miss Tanzania 2014 kuangukia kwa mwanadada Sitti Abbas Mtemvu, maneno yalizagaa sana kuwa mrembo ana miaka 18 na ana Shahada ya Uzamili (Masters).
Katika kuondoa utata, Katibu wa kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa amesema kuwa mshindi wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu amezaliwa Mei 31 mwaka 1991 na umri wake sahihi ni miaka 23 na sio miaka 18 kama ilivyozagaa sehemu mbalimbali.
Katibu huyo aliongeza kuwa Sitti ana Shahada ya ya Uhusiano wa Kimataifa na alimaliza masomo yake Desemba mwaka jana katika Chuo Kikuu cha North Texas kilichoko kwenye jiji la Dallas nchini Marekani.
Sitti Mtemvu bado hajasoma ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters) kwa sasa ila anatarajiwa kwenda kusoma ngazi hiyo huko nchini Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni