Amber Rose na Wiz Khalifa, wanandoa ambao wametengana hivi karibuni bado wanaonesha kuna mapenzi kati yao na sio maadui kama wengi walivyodhani.
Jumanne asubuhi, Wiz Khalifa alimtumia Amber Rose ujumbe wa kumtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa kupitia Twitter.
“Happy Birthday Amb,” alitweet Wiz Khalifa, ujumbe uliopokelewa vizuri kwa shukurani na Amber Rose.
“Thank u Sweetheart #IstillLoveYouNoMatterWhat.” Alitweet Amber Rose.
Mwanamitindo huyo ambaye alikuwa anatumiza miaka 31 alisherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa na marafiki zake.
Hivi karibuni Wiz Khalifa amekuwa akionekana na wasichana warembo tofautitofauti katika maeneo ya Las Vegas na Hollywood.
|
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo December 15, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam December 15,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za M...
Dakika 18 zilizopita
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni