
Ashoka Mukpo (33), mpiga picha wa gazeti la NBC News ametajwa kuwa mmoja ya watu wachache ‘waliobahatika’ kupona Ebola. Mwanahabari huyo alipata maambukizi hayo akiwa Liberia, amesema alipogundua ana dalili za maambukizi ya ugonjwa huo, alisafiri kurudi Marekani na baada ya kufikishwa hospitali alihudumiwa kwa kuongezewa damu kutoka kwa Dk. Kent Brantly, ambaye ni mmoja wa watu waliotibiwa ugonjwa huo na kupona nchini humo.

Marekani imeimarisha uchunguzi wa virusi vya Ebola katika maeneo ya viwanja vyake 5 vya ndege ambapo watu wanaoingia nchini humo wakitokea Afrika Magharibi, wanalazimika kupitia katika viwanja hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni