Jon Schultz
Mfanyabiashara mmoja ameamua kutumia ‘fursa’ aliyoiona kupitia janga la Ebola linalosumbua maeneo mbalimbali ya dunia kwa sasa, kwa kuuza domain ya www.ebola.com kwa pesa nyingi.
Jamaa huyo anayejiita ‘domain entrepreneur’ aliinunua domain hiyo miaka minne iliyopita (2008) kwa $13,500 sawa na zaidi ya shilingi milioni 22, na amedai kuwa alikuwa akisubiri wakati muafaka wa kuiuza.
“Ebola.com would be a great domain for a pharmaceutical company working on a vaccine or cure, a company selling pandemic or disaster-preparedness supplies, or a medical company wishing to provide information and advertise services” Schultz aliiambia CNBC.
Kwa mujibu wa Daily Mail, Schultz piz anamiliki domain zingine kama H1N1.com, birdflu.com, terror.com, PotassiumIodide.com, fukushima.com.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni