Social Icons

Jumatano, 12 Februari 2014

RAGE -NIMEPOKEA BARUA TATU KUTOKA FIFA, IMO INAYOMHUSU OKWI



Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), limetuma barua tatu tofauti kwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, moja ikiwa ni ile inayomhusu Emmanuel Okwi ambaye sasa yuko Yanga.
Moja ya barua ambazo Rage amepewa kopi na Fifa ni ile ambayo Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa), limemuomba Okwi kurejea Uganda na kuitumikia timu ya taifa katika michuano ya kimataifa.

Pamoja na barua hiyo, Rage amethibitisha kupokea barua hizo tatu kutoka Fifa ikiwemo ile ya Etoile du Sahel ya Tunisia kuomba kuongezewa muda wa kulipa deni la dola 300,000 wanazodaiwa na Simba kutokana na mauzo ya Okwi.

“Kweli nimepokea barua hizo, moja ni ile ambayo Etoile ambao mwezi huu ndiyo ulikuwa mwisho kulipa dola 300,000, sasa wameomba waongezewe muda hadi Septemba, mwaka huu ili waweze kulipa.
“Fifa wao wamenitumia kopi lakini barua hiyo ni kutoka kwao Etoile kwenda Fifa na wamethibitisha kwamba ni kweli Simba inawadai,” alisema Rage.
Barua ya tatu kati ya hizo kwa mujibu wa Rage ni ile ambayo inaonyesha namna klabu hiyo ya Tunisia ilivyomshitaki Okwi kwa Fifa kutokana na kuonyesha kukiuka mambo kadhaa wakati akijua mkataba wake nao unamalizika mwaka 2016.
“Katika ile barua ya kuhusiana na suala la kulipa, Fifa wametaka tusaini na kukubali kwamba sasa mwisho utakuwa Septemba 30 na tayari barua hiyo nimeikabidhi kwa Hans Pope,” aliongeza Rage.
Tayari Okwi yuko nchini na Yanga imemsajili ingawa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeamua kusimamisha usajili wake hadi litakapopata ufafanuzi kuhusiana na usajili wake.
Wakati Fifa ilitoa kibali kwa Okwi kucheza SC Villa ya Uganda kwa miezi sita, lakini Yanga ikamnunua na kuingia naye mkataba wa miaka miwili, suala ambalo limezua mzozo mkubwa huku Simba wakiendelea kusisitiza kulipwa fedha zao ambazo mwanzo walimuuza na hawakulipwa. 
Okwi amekuwa akisisitiza kwamba anataka kuichezea Yanga ambayo imemsajili, huku akieleza amekuwa akiumia moyoni kuona wenzake wakicheza naye akiwa jukwaani kama mtazamaji. 

VIONGOZI WA KINONDONI MNALIONA HILI; KITUO CHA DALADALA CHA BIAFRA CHAGEUZWA SEHEMU YA KUTUPA TAKA

Uchafu ukiwa nyuma ya kituo cha Biafra na ukitizama picha vizuri kuna abiria amekaa lakini cha kusikitisha nyuma yake kuna uchafu ambao unatoa harufu mbaya na pia kuna wafanya biashara katika eneo hili. Sehemu hii imekuwa kero kwa abiria wanaoshuka na hata wanaopanda magari kwenye hiki kituo cha Biafra kilchopo Kinondoni kwani kuna uchafu mwingi unaotupwa na wakazi wa eneo hilo mpaka kituo hiki kubadilishwa na kuwa dampo.
 Hii ndio hali halisi ya kituo cha Biafra kilichopo kwenye wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kilichogeuzwa kama sehemu ya kutupia takataka.
Jambo la kujiuliza ina maana hapa Biafra hakuna Dampo? Au uongozi wa eneo hili umelala mpaka kituo hiki kuwa na hali kama hii inasikitisha sana.

PRESIDENT KIKWETE MEETS BRITISH FOREIGN SECRETARY WILLIAM HAGUE IN LONDON TODAY


 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets British Foreign Secretary William Hague in his London office this evening. The two leaders then held talks on bilateral issues concerning their two countries.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, British Foreign Secretary William Hague and Tanzania’s Minister for Foreign Relations and International Cooperation Bernard Membe pose for a photograph shortly after they met Mr.Hague in his London office this evening.President Kikwete is in London to attend the London Conference on Illegal Wildlife Trade
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete with British Foreign Secretary William Hague in London  this evening after the  two leaders  held talks on bilateral issues concerning their two countries. 

Jumatatu, 10 Februari 2014

BOSCO NTAGANDA MAHAKAMANI ICC



Ntaganda pia anatuhumiwa kwa kuwatumia wanawake kama watumwa wa ngono
Kesi ya Bosco Ntaganda anayetuhumiwa kwa uhalifu wa kivita Katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inaanza leo katika mahakama mjini The Heague Uholanzi.
Amekana madai ya kufanya uhalifu wa kivita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo miaka kumi iliopita.
Bosco Ntaganda alijisalimisha katika ubalozi wa Marekani nchini Rwanda mwaka uliopita wakati kundi lake M23 lilipoanza kulemewa.
Ni miongoni mwa washukiwa wakuu wa ICC wanaotuhumiwa kwa kuwatumia watoto wadogo kama wanajeshi,kuwatumia wanawake watumwa wa ngono na mauaji.Chanzo BBC Swahili
Kikao cha leo kinatarajiwa kuwasaidia majaji kuamua iwapo kuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashitaka Ntaganda.

JESHI LA AUSTRALIA LAKAMATA MADAWA YA KULEVYA PWANI YA TANZANIA-GPL

Askari wa  HMAS Melbourne wakiwa na madawa yaliyokamatwa.
 Madawa hayo yakiharibiwa.

JESHI la majini la Australia limekamata na kuharibu kilo 353 za madawa ya kulevya aina ya heroin yenye thamani inayokadiriwa kuwa zaidi ya dola milioni 700 katika pwani ya Tanzania.

Askari wa meli ya HMAS Melbourne waliyagundua madawa hayo katika meli moja Jumatano iliyopita wakiwa katika shughuli za kupiga vita ugaidi na kuimarisha usalama maeneo ya baharini Mashariki ya Kati na Bahari ya Hindi.

Mkuu wa kikosi hicho, Daryl Bates, alisema hatua hiyo ilikuwa ni pigo katika kukwamisha njia za kupatikana kwa fedha zinazotumiwa na magaidi.

IRINGA NA DSM NAKO MADUKA YAFUNGWA KUKWEPE KUTUMIA MASHINE ZA TRA


 Hapa ni maeneo maarufu ( kama mtaa wa congo dar) sana mkoani Iringa,panajulikana kama Miyomboni kukiwa kimya kutokana maduka yote ya bidhaa muhimu yamefungwa na wananchi wanaendelea kupata taabu kutokana na mgomo wa kutumia mashine za kutolea risiti za TRA.
(picha na Denis Mlowe )

WENYE MADUKA KARIAKOO 

Baadhi ya maduka ya wafanyabiashara kariakoo yaliyofungwa
Wafanyabishara ambao wanamiliki maduka maeneo yote ya kariakoo leo asubuhi wameweka mgomo wa pamoja wakutofungua maduka yao wakipinga uamuzi wa TRA kutaka kila duka kuwa na mashine.
Mitaa yote ya Kariakoo, Msimbazi, Uhuru, Lumumba, Aggrey, Mchikichi, Narung’ombe, Tandamti, Congo, kote maduka yamefungwa baada ya kutangaziwa na umoja wa wafanyabiasha.
Wafanyabishara wanapinga bei kubwa ya mashine ambayo ni milioni moja mpaka lakini nane.

TAARIFA YA WIZARA YA MAMBO YA NJE KUHUSU WAFUNGWA WA KITANZANIA NCHINI CHINA


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kukanusha taarifa za uvumi zinazosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo vya habari kuwa kuna Watanzania wapatao 160 wamenyongwa nchini China kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya.
Wizara inapenda kuujulisha Umma kuwa hakuna Mtanzania yeyote aliyenyongwa kama inavyodaiwa kwenye mitandao na vyombo vya habari.
Aidha, taarifa hiyo ya uvumi imedai kuwa ndugu wa mmoja wa Watanzania hao ambaye kwa jina anajulikana kama Bw. Rajab Mohamed Ismail Mapusa wamekaa matanga kuomboleza kifo chake.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Serikali ya China, Bw. Mapusa yupo hai gerezani akitumikia kifungo cha maisha kwa kosa la kuingiza madawa ya kulevya nchini humo, na hivi karibuni alishiriki kuandaa maonyesho ya utamaduni wa Kiafrika wakati wa kuadhimisha sherehe za Mwaka Mpya wa China.

Jumatano, 5 Februari 2014

ICC:NINI HATMA YA KESI YA KENYATTA?


Rais Kenyatta na wakili wa Naibu Rais William Ruto Karim Khan
Hatma ya kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC, inatarajiwa kuamuliwa leo Jumatano, wakati ambapo viongozi wa mashitaka katika mahakama hiyo wataoomba muda wa ziada kujiandaa kwa kesi.
Mawakili wa Kenyatta wanatumai kuwa kesi hiyo ambayo imezua mgawanyiko kati ya mataifa ya Afrika itatupiliwa mbali.
Mataifa ya Afrika yamekuwa yakikosoa ICC kwa kulenga tu viongozi wa Afrika.
Kesi dhidi ya Kenyatta ni muhimu kwa ICC ambayo imefanikiwa tu kumhukumu mtu mmoja huku nyingi ya kesi zinazofikishwa katika mahakama hiyo zikitupiliwa mbali kutokana na sababu nyingi tu tangu kubuniwa miaka 11 iliyopita.
Wadadisi wanasema kuwa huenda kesi hiyo ikaleta msukosuko katika kanda ya Afrika Mashariki ikiwa viongozi wa mashitaka watasisitiza iendelee.
Rais Kenyatta alifikishwa ICC kutokana na tuhuma kuwa alikuwa mmoja wa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2007/2008. Anakabiliwa na makosa ya mauaji na uhalifu mwingine dhidi ya binadamu.
Kadhalika Kenyatta alishitakiwa pamoja na makamu wake wa Rais William Ruto kwa tuhuma sawa. Kesi dhidi ya Ruto inaendelea katika mahakama hiyo.
Mataifa ya Magharibi ambayo yanajitolea katika kuunga mkono ICC, pia yana wasiwasi kuhusu uhusiano wao na Kenya ambayo inaonekana kama mshirika mkubwa katika vita dhidi ya kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia.
Watu 1,200 walipoteza maisha yao katika ghasia za uchaguzi mkuu mwaka 2007/08 huku maelfu wakilazimika kutoroka makwao. Wote wamekanusha mashitaka.
Viongozi wa mashitaka ICC wanasema kuwa Kenyatta aliongoza ghasia hizo lakini kesi dhidi yake imefanywa dhaifu kutokana na baadhi ya mashahidi kujiondoa katika kesi hiyo tangu kesi hiyo kuwasilishwa katika mahakama hiyo miaka minne iliyopita.
Kesi yenyewe ilitarajiwa kuanza Jumatano, lakini ikaahirishwa kwa mara ya nne mwezi jana wakati ambapo wendesha mashitaka waliposema kuwa shahidi mwingine alijiondoa kwenye kesi huku wakiomba mahakama kuwapa muda zaidi kutafuta ushahidi.
Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mashahidi wengi wamehongwa au kutishwa kiasi cha kujiondoa katika kesi hiyo.Chanzo BBC Swahili

BASI LA ZUBERI LAPATA AJALI MKOANI SINGIDA MCHANA NA KUUA WANNE HAPO HAPO


ajali-singida1
Picha hii haihusiki na ajali ya basi la Zuberi iliyotokea mchana huu huko wilayani Ikungi.


BASI la Zuberi lenye namba T119 AA2 limepata ajali mbaya katika kijiji cha Nkuhi wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida na watu wanne wameripotiwa kufa papo hapo kwa kukatwa vichwa huku majeruhi wengi wakiwa wameumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili.

Akizungumza na MOblog kutoka eneo la tukio leo mchana huu, mwandishi wa habari, Nathanieli Limu  amesema basi hilo la Zuberi lilikuwa linatoka Mwanza kuja Dar na lilikuwa na zaidi ya abiria 60.

Amesema kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa basi hilo alikuwa anajaribu kumkwepa bibi kizee aliyekuwa anakatisha barabarani kwenye majira ya saa saba mchana.

“ilikuwa si ajali ya kawaida baada ya bibi kizee kukatiza barabarani na wakati dereva anajaribu kumkwepa alirudi mara ya pili barabarani ndipo hapo gari lilipinduka na kuanguka kwenye mtaro,” amesema Limu

Alilisitiza kwamba mashuhuda wa ajali hiyo wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikiana baada ya bibi huyo kuamua kurudi mara ya pili barabarani na kusababisha ajali na kukaa kwa muda mrefu eneo la tukio.

Amesema kwa basi hilo la Zuberi liliinuliwa na lori lenye kifaa maalumu cha winch baada ya basi hilo kumlalia mtoto mdogo wa miezi kadhaa ambaye mama yake ni miongoni mwa waliofariki dunia papo hapo na maiti yake kupelekwa hospitali ya mkoa wa Singida.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA MH:MWIGULU AHITIMISHA ZIARA YAKE YA MIKOA MITATU KWA KUZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA MBEYA MJINI


Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wafanyabiashara wa Mbeya Mjini hii leo kwenye Ukumbi wa Mtenda Hotel Jijini Mbeya.Sehemu ya Wafanyabiashara wa Mbeya Mjini wakiwa kwenye Mkutano wa ndani wa Naibu Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba hii leo.
 
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba hii leo amehitimisha ziara yake ya kikazi iliyojumisha Mikoa Mitatu(Njombe,Ruvuma na Mbeya),Ziara yake imehitimishwa kwa Kuzungumza na Wafanyabiashara wa Mbeya Mjini,Pia amekutana na Watendaji/watumishi wa Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA),Hazina ndogo Mkoani Mbeya na Ofisi ndogo ya Takwimu.
Akizungumza na Wafanyabiashara wa
Mbeya Mjini Naibu Waziri  amesema,Katika ziara yake amesisitiza kuwa Ofisi yake inatambua Mchango wa Wafanyabiashara katika Uchumi wa Nchi hii hususani ulipaji wa kodi,Hivyo katika utungaji wa Sera mbambali za ulipaji kodi na Kuinua Uchumi wa Nchi, Ofisi yake itashirikiana na Wafanyabiashara  nchi nzima kwasababu ndio wadau husika kwenye ulipaji kodi katika Taifa hili.

Pia Mh:Mwigulu ameendelea kuwaomba Wafanyabiashara kuendelea kuunga mkono matumizi ya Mashine za EFD's kwenye ukusanyaji wa kodi halisi za bidhaa/huduma husika inayotolewa.Ni muhimu kwa Watanzania kutambua mabadiriko ya mifumo ya ukusanyaji kodi nchini kwa manufaa yao na Taifa lao,Kutumia mashine za EFD's kunasaidia kudhibiti upotevu wa mapato kupitia kodi,Kunasaidia wafanyabiashara kupata makusanyo stahiki kulingana na huduma/bidhaa anazouza.
Akiwa ameambatana na Wataalamu kutoka Wizarani na Makao Makuu ya TRA,Wafanyabiashara wa Mbeya wameelimishwa kuwa Mfanyabiashara yeyote mwenye mauzo kuanzia Milioni 14 kwa Mwaka ndiye anapatwa kutumia mashine hizo,Pia wafanyabaishara wote waliosajiliwa kulipa kodi,Pia matumizi ya Mashine za EFD's zinasaidia kutunza kumbukumbu za biashara husika,Zinapunguza wizi na Ujanja wa  wauzaji wasio wenye mali.
Vilevile,Wafanyabiashara wa Mbeya wameomba serikali kuondoa ufutiliaji wa kulipa kodi kwa wachuuzi wadogowadogo,Serikali ifanyie kazi Ukusanyaji wa Kodi kwenye Viwanda,Mipakani,Viwanja vya ndege na kwenye Soko la kimataifa.Pia sheria ya Kodi ni kandamizi kwa Wafanyabiashara wa dogowadogo na faini zake ni kubwa mno kitu kinachoshawishi Rushwa kati ya Wafanyabiashara na Watendaji wa TRA.

NAIBU WAZIRI KITWANGA APOKEA SHEHENA YA MWISHO YA MABOMBA YA MWISHO KATIKA BANDARI YA MTWARA

 Naibu Waziri Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Mhe. Charles Kitwanga (wa tatu kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Menjeja wa Bandari  ya Mtwara (wa pili kutoka kushoto) Bw. Absalim Bohella. Anayefuatia ni  Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Wilman Kapenjama Ndile, na uongozi wa Mkoa mara baada ya kupokea Shehena ya mwisho ya Mabomba ya Gesi katika  bandari ya Mtwara.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara wakiendelea na kazi ya kupakua 
shehena ya mabomba ya gesi kutoka katika meli baada ya mabomba hayo  kuwasili katika Bandari ya Mtwara.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara wakiendelea na kazi ya kupakua 
shehena ya mabomba ya gesi kutoka katika meli baada ya mabomba hayo  kuwasili katika Bandari ya Mtwara.
 Mtaalamu wa Masuala ya Gesi na Msimamizi Mkuu wa Mitambo ya Kusafisha Gesi 
Mhandisi Sultan Pwaga (katikati) akimweleza jambo Naibu Waziri wa  Nishati na Madini Mhe. Charles Kitwanga na ujumbe wake alipotembelea  eneo hilo kuangalia namna shughuli mbalimbali zinavyoendelea katika eneo hilo.
Naibu Waziri Mhe. Charles Kitwanga (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Wilaya
ya Mtwara Mhe. Wilman Kapenjama Ndile, (wa kwanza kulia) wakipata   maelezo kutoka kwa mtaalamu Abshakim Marunda kuhusu namna kisima cha  gesi cha nchi Kavu kinavyofanya kazi. Kwa mujibu wa Maelezo ya Mjiologia Mwandamizi wa TPDC Bw.George Ngwale hayupo pichani ameeleza kuwa, Mnazi Bay ina jumla ya visima vitano kati ya hivyo visima vine vina gesi  inayochimbwa na kisima kimoja kikavu. Aidha gesi inayopatikana katika  eneo hili inauzwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambao wanatumia  kuzalisha umeme unaosambazwa katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. Wa kwanza  kushoto ni Katibu wa Mhe. Naibu Waziri Bw. Mjengwa Ngereja.


Na Asteria Muhozya, Mtwara

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Mhe. Charles Kitwanga, amepokea Shehena ya mwisho ya mabomba ya gesi katika bandari ya Mtwara na kueleza kuwa, ujio wa miundo mbinu hiyo ni neema kwa uchumi wa Tanzania.

Aliongeza kuwa, hiyo ni hatua kubwa katika kufikia malengo tarajiwa ikizingatiwa kwamba, kukamilika kwa mradi huo kutachochea na kufungua njia mbalimbali za uchumi unaoendana na sekta ya gesi na mafuta.

“Ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha gesi ni jambo jema kwa Tanzania, tunataka kuingia katika uchumi wa kati wa dola elfu tatu au karibu ya hapo, tunataka pato la mtanzania liongezeke. Sasa bila kuwa na umeme haya yote hatutayafikia. Gesi itazalisha mengi, tunataka tufikie lengo letu. Alisema.’’ Mhe. Kitwanga.

Aidha, aliongeza kuwa, kuzalishwa kwa gesi  na kusambazwa katika maeneo mbalimbali chini kutasaidia kufungua fursa nyingi ikiwemo  kuongezeka kwa viwanda ambavyo vitakuwa na uhakika  wa kupata umeme unaotokana na gesi.

Vilevile, alieleza kuwa, mbali na matumizi ya viwandani gesi inatarajiwa kutumiwa katika mahitataji mbalimbali yakiwemo matumizi ya majumbani.

 “Nataka kuwaeleza wana Mtwara, si kwamba gesi itachukuliwa yote, hapana. Tunachotaka kufanya ni kuisambaza maeneo mbalimbali lengo letu ni kukuza uchumi wetu kwa kutumia gesi hata Mtwara viwanda vitajengwa na fursa mbalimbali zitakuwepo”. Alisema.

Akieleza mafanikio ambayo yamekuwepo kutokana na shughuli za gesi kutumia bandari ya Mtwara, Meneja wa Bandari Bw. Absalim Bohella alieleza kuwa, ujio wa gesi na mradi unaotekelezwa Mkoani humo umekuwa neema kwa bandari hiyo kutokana na kuongezeka kwa mapato yanayotokana na bandari hiyo pia  kutumiwa kwa shughuli mbalimbali za gesi.

Aliongeza kuwa, tayari bandari ya Mtwara imevuka malengo ya ukusanyaji
mapato waliojiwekea ambapo hadi sasa tayari zaidi ya Tsh. Milioni mia tano kimekusanywa. Aidha, aliongeza kuwa, mradi wa gesi umewaongezea watumishi wa bandari hiyo ujuzi kutokana kufanya shughuli tofauti tofauti zinazohusiana na gesi ikiwemo upakuaji wa bidhaa zinazopitia katika bandari hiyo kwa shughuli.

“Bandari bila rasilimali watu si kitu. Kwa wafanyakazi waliobobea wamepata ujuzi zaidi na sasa wanao uwezo wa kuhudumia shughuli zote za bandari”. Aliongeza.

Akielezea hatua mbalimbali ambazo zimefikiwa katika ujenzi wa miundombinu ya gesi, Mtaalamu wa Masuala ya Gesi na Msimamizi Mkuu wa Mitambo ya Kusafisha Gesi Mhandisi Sultan Pwaga alieleza kuwa, shughuli za uwekaji mabomba ya gesi unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Julai, 2014 ambapo pia inatarajiwa mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka huu shughuli za usimikaji mitambo utakamilika.

 Vile vile, ameongeza kuwa, shehena hiyo iliyopokelewa katika bandari ya Mtwara ni ya mwisho lakini mabomba ya mwisho ya mradi yatapokelewa tarehe 10 Februari, 2014 katika bandari ya Dar es Salaam.

Aidha, aliongeza kuwa, miundombinu hiyo ndio kichocheo cha gesi asilia
na lengo la mradi huo ni kuhakikisha kuwa, mitambo inajengwa mahali ambapo gesi asilia inachimbwa.

Mbali ya kupokea Shehena za mabomba ya mwisho ya gesi, Mhe. Kitwanga
ametembelea eneo la Mnazi Bay ambako gesi asilia na kuuzwa katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambapo shirika hilo linaitumia gesi hiyo kuzalisha umeme kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Vilevile, Mhe. Kitwanga alitembelea katika eneo la Madimba kunakojengwa
kambi za wafanyakazi na panapotarajiwa kujengwa mitambo ya kusafisha gesi.
 
 
Blogger Templates