Social Icons

Jumapili, 27 Oktoba 2013

SAD NEWSS! WEMA SEPETU AMEONDOKEWA NA BABA YAKE MZAZI(AMEFARIKI)


Muigizaji, mrembo maarufu nchini Tanzania (Miss Tanzania 2006),Wema A. Sepetu, amepatwa na msiba mkubwa. Amefiwa na Baba yake mzazi,Balozi Isaac Abrahamu Sepetu.
mzee Sepetu akiwa hospitali 
Taarifa zinasema kwamba Mzee Sepetu ambaye kwa muda wa miezi kadhaa sasa amekuwa akiugua na kusumbuliwa na maradhi ya kiharusi,. Mzee Sepetu alikuwa pia akisumbuliwa na kisukari.Amefariki jijini Dar-es-salaam. Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.
Wema katika picha ya pamoja na baba yake mzazi,Balozi Abraham Sepetu. Pembeni ni rafiki wa karibu wa Wema,Petitman



                                                      Balozi Issac Abraham Sepetu
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarag Nyerere. Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere.

Pia, Machi 27, mwaka huu, Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dr Mohammed Shein, kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitegauchumi ya Zanzibar (ZIPA).
onaviews.blogspot.com anaungana na waombolezaji wengine wote katika kipindi hiki kigumu... Bwana alitoa na Bwana ame twaa Amen.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates