Wafuasi wa Morsi wakabiliana na polisi Misri
Vikosi vya usalama nchini Misri vimeimarisha ulinzi katika
sehemu kadhaa mjini Cairo baada ya vurugu kuzuka kutokana na makabiliano kati ya
wafuasi wa Mohammed Morsi na vikosi vya usalama katika mji huo na ule wa
Alexandria.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo Quentin Sommerville anasema kuwa milipuko na milio mikuwa ya risasi imesikika katika sehemu za katikati mwa mji mkuu.
Sehemu ambazo zimezingirwa ni kama vile ambako wafuasi wa rais aliepindiliwa
Mohammed Morsi waliwahi kupiga kambi baada ya Morsi kuondolewa kwa nguvu
mamlakani na vikosi vya usalama mwezi Agosti katika operesheni iliyosababisha
mamia kadhaa kupoteza maisha.
Pia usalama umeimarishwa karibu na medani ya Tahrir ambako waandamanaji waliokuwa wanapinga Morsi walikusanyika katika maandamano ya kumtaka ajiuzulu kabla ya majeshi kumtoa madarani miezi mitatu iliopita.
Vyombo vya habari vimeripoti kutokea ghasia zaidi katika mkoa wa Kaskazini wa Sharqiya, Mashariki mwa Giza, pamoja na Kaskazini mwa mji wa bandarini wa Alexandria.
Mamia ya watu wameuwa tangu jeshi kumuondoa mamlakani Morsi mwezi Julai.
Maelfu ya wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood pia wamezuiliwa katika miezi miwili iliopita.
Baadhi ya maafisa wakuu wa chama hicho akiwemo bwana Morsi na generali Mohammed Badie, wanazuiliwa kwa madai ya kuchochea ghasia na mauaji.
Vuguvugu hilo limelalamika na kusema kuwa maafisa wanazifanya juhudi zao dhidi yaokuonekana kama vita dhidi ya ugaidi

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni