Social Icons

Alhamisi, 24 Oktoba 2013

SOMA HABARI YA KOBE WA AJABU ANAYE VUTA SIGARA 10 KWA SIKU

Meet-A-Turtle-That-Smokes-10-Cigarettes-A-Day.jpg2
Maajabu hayaishi duniani na kila siku yanajitokeza maajabu mapya ambayo hukuwahi kutarajia kuyashuhudia maishani mwako . Nchini Japan kuna kobe ambaye amejiingiza kwenye tabia ya uvutaji wa sigara na mpaka sasa anavuta sigara kumi kwa siku.



Kobe huyu alianza tabia ya kuvuta sigara wakati mmiliki wake Bwana Tang alipojaribu kuutoa mfupa wa kuku uliokuwa umekwama tumboni mwa kobe huyo .
Snapping turtle addicted to smoking smokes 10 cigarettes a day, Changchun, Jilin Province, China - 28 Jun 2013
Kobe alimg’ata wakati jamaa alipojaribu kuingiza mkono wake kinywani mwa kobe , Mr Tang aliamua kuiweka sigara aliokuwa akiivuta yeye mwenyewe mdomoni mwa kobe ili kumziba asimng’ate tena . Kobe aliivuta sigara ile huku akiutoa moshi mdomoni kama kawaida na ndani ya dakika tatu ilikuwa imeisha na mpaka sasa imekuwa tabia na kobe huyo anavuta mpaka sigara kumi kwa siku moja . Mr Tang anatafuta njia ya kumuachisha kobe tabia hiyo ya uvutaji sigara.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates