Social Icons

Jumanne, 22 Oktoba 2013

DRC na M23 wasitisha mazungumzo.


Waasi wa M23 wanaolalamikiwa kuvuruga amani ya Mashariki ya Kongo

Mazungumzo ya amani kati ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23 yamesitishwa tena licha ya Umoja wa Mataifa kuweka msukumo wa kuendelea kwa majadiliano ya pande hizo mbili.

Mazungumzo hayo yamekuwa yakiendelea mjini Kampala Uganda tangu Septemba mwaka huu ambapo kila upande umetoa tamko lake kuhusiana na kusitishwa kwa mazungumzo hayo.
Msemaji wa Serikali ya Kongo Lambert Mende amesema kuwa mazungumzo yamesitishwa kutokana na kutofikiwa makubaliano kuhusu msamaha kwa M23 na jinsi watakavyo jumuishwa katika jeshi la Taifa la nchi hiyo FARDC.

Mjumbe wa M23 katika mazungumzo hayo Roger Lumbala alisema kumekuwa na vikwazo lakini wao wako tayari kurejea kwenye meza ya majadiliano wakati wowote.

Awali serikali ilionya kuwa majadiliano yaliyoanza upya mwezi Septemba chini ya shinikizo la Viongozi wa nchi za Maziwa Makuu yalikuwa yanakwenda taratibu mno hali iliyoashiria mwisho wa maafikiano.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates