Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya kidemokrasi
ya Congo, ameambia baraza la usalama la Umoja huo kuwa makali ya kundi la waasi
la M23 kama tisho la kijeshi yamekwisha
Martin Kobler alisema kuwa kundi hilo limeondoka katika maeneo yao ya kivita
mashariki kwa DRC, na kwamba sasa wako katika eneo dogo karibu na mpaka wa
Rwanda.
Waasi hao wanasema kuwa wameondoka katika maeneo yao ya vita kwa muda.
Aidha bwana Kobler aliambia baraza al usalama kupitia kwa njia ya Skype kuwa
kwa sasa ni kama kundi ilo limefika mwisho wake.
Aliongeza kwamba waasi wameondoka katika ngome yao moja kuu ya mlima Hehu
karibu na mpaka wa Rwanda.
Baada ya mkutano huo, balozi wa Ufaransa Gerard Araud alisema anatumai
kutakuwa na mazungumzo sasa kati ya waasi hao na serikali.
Alisema: ‘‘Bwana Kobler ametuarifu kuwa wanashuhudia mwisho wa kundi la M23
kama tisho la kijeshi. Kwa hivyo naona kama ni hatua nzuri na kwamba hata
kulikuwa na makubaliano kuwa sasa tushinikize mazungumzo kuanza tena mjini
Kampala.’’
Mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi wa M23, mjini Kampala,
yalisitishwa wiki jana.
Hali hata hivyo hali ilikuwa imetulia Mashariki mwa DRC kwa muda wa wiki
moja.
Watu walionekana wakishangilia wakati wanajeshi walipoingia mji wa Rumangabo
ambao ulikuwa umetekwa na waasi hao
Na sasa serikali inadhibiti hali mjini humo, kwa mujibu wa gavana wa jimbo la
Kivu Kaskazini, Julien Paluku.
‘‘Tumekuwa na mikutano miwili ili kujadili tutakavyoimarisha hali ya
wananchi...na tutatangaza kuanza tena kutolewa kwa huduma za serikali katika
muda wa masaa 24,’’ alisema Paluku.
Mji wa Rumangabo – ulio umbali wa kilomita 50 Kaskazini mwa Goma, mji rasmi
wa Mashariki mwa DRC, ulikuwa na kambi tatu kubwa za kijeshi nchini humo kabla
ya kutekwa na waasi wa M23 mwaka jana.
Hapana shaka kuwa majeshi ya serikali yamefikia hatua kubwa na kupata ushindi
mkubwa dhidi ya waasi,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni