MWANAMKE: JE UNATAFUTA MCHUMBA? FUATA KANUNI HII, HAKIKA UTAMPATA MCHUMBA MWENYE TABIA UZITAKAZO
Mwanamke: Je, unatafuta mchumba? Fuata kanuni hii hakika utapata mchumba mwenye tabia uzitakazo...
Kuna kitu kinaitwa nguvu ya mvuto, lakini pia huenda mmeshawahi kusikia au kusoma kitabu kinachoitwa “The Secret.” Ni kitabu kizuri sana kinachoeleza kwa kirefu na kwa lugha nyepesi inayoeleweka jinsi nguvu hii ya mvuto inavyofanya kazi. Katika kitabu cha The Secret mwandishi Rhonda Byrne anasema kwamba mawazo yetu ni kama sumaku. Kwa kawaida sisi wanadamu tumezungukwa na nguvu ambazo hatuzioni lakini zipo kwa hiyo Kwa jinsi tunavyofikiri hayo mawazo yanakuwa na nguvu ambazo zinavuta kila kitu tunachowaza, kiwe kizuri au kibaya, ni lazima kitarudi kilipotoka, ambapo sipengine bali kwako wewe mwenyewe.
Rhonda anazidi kubainisha utendaji wa mawazo yetu kwa kutoa mfano wa ufanyaji kazi wa Luninga (TV). Kama wote tunavyofahamu kuwa ili kituo cha kurusha matangazo ya Luninga kifanye kazi kunakuwa na minara inayosafirisha mawimbi na kuyageuza katika mfumo wa picha na hivyo kutuwezesha kuona matangazo ya luninga tukiwa majumbani kwetu. Wengi wetu hatufahamu mitambo hiyo inafanya kazi namna gani, lakini tunafahamu kwamba kila chaneli ina mawimbi yake ambapo kila tukichagua chaneli fulani tunapata picha katika luninga zetu. Tunachagua mawimbi kwa kubadilisha chaneli na ndipo tunapopata picha za matangazo kutoka katika chaneli hiyo. Kama tunataka kuona picha na matangazo tofauti katika luninga zetu tunabadilisha chaneli kwa kutafuta mawimbi ya chaneli nyingine.
Sisi kama wanaadamu tuko sawa na mnara wa kurusha matangazo ya luninga na tuna nguvu kuliko minara ya kurusha matangazo iliyowahi kuwepo hapa duniani. Mawimbi yetu ndiyo yanayoratibu maisha yetu na ndiyo yanayoifanya dunia iwe kama livyo leo, kwani tunatengeneza mawimbi kutokana na namna tunavyowaza. Ile picha tunayopata au tunayoiona kupitia mawazo yetu, sio sawa na ile tunayoiona katika luninga zetu sebuleni kwetu, bali ni picha ya maisha yetu! Mawazo yetu yanatengeneza mawimbi na yanavuta kila tunachokiwaza na kuwa ndio maisha yetu halisi.
Iwapo tunataka kubadili chochote katika maisha yetu, basi inatulazimu tubadili chaneli na mawimbi kwa kubadili namna yetu ya kufikiri. Mwandishi huyo anaendelea kusema, kinachosabisha watu wengi wasipate kile wanachokitaka maishani ni kwa sababu wanafikiria zaidi kuhusu kile wasichokitaka badala ya kile wanachokitaka. Hebu tujaribu kuchunguza mawazo yetu na kauli zetu, tutagundua siri kubwa. Kwani nguvu ya mawazo ipo na inafanya kazi. Ugonjwa mkubwa sana unaowakabili wanadamu hapa duniani karne kwa karne ni ugonjwa wa “sitaki” au “sipendi,” anabainisha mama huyo. “Watu wameendelea kuacha ugonjwa huu uendelee kutawala katika mawazo yao, vitendo vyao na kauli zao, wakiendelea kuzingatia yale wasiyoyataka au wasiyoyapenda.” Anamalizia kusema mwandishi huyo.
Ugonjwa huo ndio unaowatesa baadhi ya wanawake wanaotafuta wapenzi. Mfano halisi ni kauli kama, “mimi sipendi wanaume wafupi,” au “mimi sipendi kuolewa na mwanaume mnyanyasaji….” na kauli nyingine zinazofanana na hizo. Ukweli ni kwamba kitakacho watokea wanawake wenye kutoa kauli kama hizo ni kuishia kuolewa na wanaume wa aina hiyo….. kinachofanyiwa kazi na mawazo yetu ya kina (Unconscious Mind) ni kile tunachokitamka, iwe ndicho tunachokitaka au tusichokitaka, mawazo yetu ya kina hayajui neno sipendi au sitaki, hukuletea kile ulichokitamka na kukijaza katika akili yako.
Kuna wanawake wengi ambao wameolewa au wamewahi kujenga mahusiano na wanaume ambao waliwahi kutamka hadharani kwamba kamwe hawatoweza kujenga mahusiano nao au kuolewa nao. Hayo ni matokeo ya kauli zao ambazo walizitamka bila kujua madhara yake. Kwa hiyo basi kwa kutumia kanuni hiyo ya mvuto kama alivyosema mwandishi Rhonda Byrne mnatakiwa kuanza kuratibu mawazo yenu na kauli zenu kwa kutamka aina ya wanaume ambao mngependa kujenga mahusiano nao au kuolewa nao na haiishii hapo ni vyema mkajiweka katika mazingira ambayo yatawavuta kuelekea mahali ambapo mtakutana na aina ya wapenzi muwatakao. Huwezi tu kukaa nyumbani kwako au kutembelea eneo moja hilo hilo kila siku halafu utarajie kukutana na aina ya mpenzi umtakaye itakuwa ngumu, labda uwe na bahati sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni