Ni muhimu sana kwako mwanaume kujua kwa uhakika kuwa mwanamke anakupena kweli kweli,utajuaje kuwa mwanamke anakupenda? Zifuatazo ni ishara ambazo wewe kama mwanaume unapaswa uwe makini ili uweze kuziona na kuzifanyia kazi;
1. Mwanamke anayekupenda atakuwa tayar kujitoa muhanga kwa ajir yako yaan kujitoa kafara,vipo vitu ambavyo watu hawawez kuvifanya ila icpokuwa kwa wale wanaowapenda kwa moyo wote. Je ww ni sehemu mojawapo ya vitu vichache anavyovipa kipaumbele?,je ww unakuwa wa kwanza mbele ya rafiki zake?,je anakufanyia vitu ambavyo hawez kuwafanyia wanaume wengne?,je ameacha mambo mengine ili aweze kuwa na ww?,ni kwa vitu kama hivi unaweza kutambua ww ni wa muhimu kwake.
2. Mwanamke anayekupenda atahangaika juu yako,mtu anayekupenda atahangaika juu ya usalama wako,raha yako,heshima yako na maendeleo yako.Hii ni moja kati ya ishara kubwa kuwa mwanamke uliyemlenga anakupenda kwel.
3. Mwanamke anayekupenda atakuonea wivu mara kadhaa,ingawaje wivu mara nyngne unaweza kuvuruga penz endapo utazidi.Wivu ni ishara kuwa anakupenda ww na anataka akulinde usiibiwe au asije akakupoteza,anaogopa usije ukatoka katika maisha yake,au kwa maneno mengine usije ukamtoa moyoni mwako na nafas yake ikachukuliwa.
4. Mwanamke anayekupenda atakapokuwa mbele ya marafiki zake au watu wengine atacheka nao lakini atakugeuzia ww macho namaanisha uso wake haraka sana. Kufanya hivi ni kuonyesha kuwa anakuhesabia ww kuwa utaweza kumletea furaha katika maisha yake,zaidi ya hilo ni kwamba anatumaini kuwa utamuona kuwa yeye ni mtu aliye rahisi kufurahishwa kwa kuwa yeye ni mtu wa furaha.
5. Mwanamke anayekupenda ataendelea kukuangalia usoni kwa muda mrefu kuliko ilivyo kawaida ya wanawake wengine,mara nyingi atakuangalia na kutabasamu vizuri. Hii huenda ni ishara moja muhimu sana ya kukuambia kuwa " ANAKUHITAJI".
6. Mwanamke anayekupenda atajitahidi apendekeze kwa kuvaa vizuri pale anapojua kuwa atakutana na wewe,atajali sana juu ya nywele zako,nguo zake na hata anavyonukia,yaani atajipulizia pafyumu.
7. Mwanamke anayekupenda ataonyesha dalili za kupenda kuwa karibu yako katika mazungumzo au maeneo mengine,atapenda mara nyingi kuwepo katika maeneo unayopendelea na pia sauti yake itabadilika kuashiria hali ya kukupenda na kutaka kukuvuta kwa sauti yake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni