Rais wa Gambia amesema kuwa bado analiongoza taifa hilo la Afrika magharibi baada ya vikosi vyake vya usalama kutibua jaribio la mapinduzi.
Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.
Hatahivyo hajulikani aliko.Milio mikali ya riasi ilizuka karibu na makao ya rais katika mji mkuu.
Bwana Jammeh alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mwaka 1994 na wapinzani wake wamekuwa wakimkosoa kwa uongozi wake wa kiimla.
Duru za kidiplomasia na zile za kijeshi zinasema kuwa wanajeshi kutoka kwa jeshi la ulinzi wa rais wanadaiwa kufanya shambulizi hilo katika makao ya rais mjini Banjul mapema siku ya jummane.
Serikali imekana kwamba kulikuwa na jaribio la mapinduzi katika taarifa iliotangazwa katika radio ya taifa.
Hatahivyo,bwana Jammeh baadaye alikiri kuhusu shambulizi hilo na kusema kuwa wanajeshi waaminifu wa Lamin Sanneh aliyemtaja kama mwenye aibu walivamia mji mkuu wa Gambia kutoka Senegal katika jaribio la kutaka kuipindua serikali yake.
Amesema kuwa wavamizi hao hatahivyo walikabiliwa na vikosi vya usalama na kuwaua wanne kati yao huku wengine wanne zaidi wakikamatwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni