Baada ya kuwepo kwa taarifa zisizothibitishwa rasmi za kufukuzwa kazi kwa kocha mkuu wa timu ya Dar es salaam young African Mbrazil Marcio Maximo, hatimae hii leo uongozi wa timu hiyo umemtangaza rasmi Mdachi Hans Van Der Pruijm kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.Tetesi za kufukuzwa kwa Maximo zilitawala vyombo vingi vya habari nchini baada ya kuwasili kwa kocha Pruijm siku ya jumatatu na kunaswa na kamera zetu akipokelewa na viongozi wa Yanga.
Taarifa ya klabu ya yanga iliyosomwa na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro mbele ya waandishi wa habari, imemtaja Hans Van Pruijm kuwa kocha mkuu wa yanga akisaidiwa na Boniface Mkwasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni