Social Icons

Alhamisi, 25 Desemba 2014

TUME OPERESHENI TOKOMEZA KUKUSANYA MAONI MIKOA YA KASKAZINI NA KATI JANUARI 2015


Na. Mwandishi Wetu Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza  itakusanya taarifa na kupokea malalamiko yaliyotokana  na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili Nchini  mikoa ya Mikoa ya Arusha, Manyara, Tabora, Singida na  Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 24 Desemba,  2014 na Katibu wa Tume hiyo, Bw.Frederick Manyanda,  Tume inatarajiwa kuendelea na zoezi la kukusanya maoni  na taarifa kuanzia tarehe 5 Januari , 2015 mpaka tarehe 21 Januari,2015 katika maeneo mbalimbali ya kanda ya  Kaskazini na Kati Nchini.

Katika kutekeleza jukumu hilo, Bw. Manyanda ameeleza kuwa, Tume itatembelea Mkoa wa Tabora tarehe 4 Januari  2015 mpaka tarehe 8 Januari 2015 na itakuwa Mkoa  wa Singida tarehe 9 Januari,2015 mpaka tarehe 10 Januari,2015.

Aidha Tume itatembelea Mkoa wa Dodoma tarehe 11  Januari, 2015 mpaka tarehe 12 Januari 2015. Vilevile,  Wakili Manyanda ameeleza kuwa Tume itakusanya maoni 

Mkoa wa Manyara kuanzia tarehe 13 Januari, 2015 mpaka tarehe 16 Januari, 2015 na Tume itakuwa Mkoa wa Arusha tarehe 16 Januari 2015 mpaka tarehe 19 Januari,2015.

Mpaka sasa Tume ya Rais ya Operesheni Tokomeza imefanikiwa kukusanya taarifa na kupokea malamiko  yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza  katika mikoa kumi na tano (15) ya Tanzania Bara ambayo ni Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mwanza Mara,Lindi,Mtwara,Ruvuma,Iringa, Morogoro.Pamoja na mikutano hiyo, Bw. Manyanda ametumia fursa  hiyo kuwakumbusha na kuwaomba wananchi na watanzania  wa maeneo husika kuendelea kutuma taarifa na  malalamiko kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza  kwa njia ya barua, simu na barua pepe ambapo ameeleza  kuwa wananchi wanaweza kutuma barua kwa Katibu wa  Tume, Tume ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza  Ujangili, SLP 9050, Dar es Salaam na barua pepe kwenda  opereshenitokomeza@agctz.go.tz.Aidha, wananchi wa  maeneo husika wanaweza kutuma ujumbe mfupi wa  maandishi kwa namba za simu za Tigo: 0714 826826; 

Vodacom: 0767 826826; Airtel: 0787 826826; na Zantel:
0773 826826.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates