Alan Pardew ametajwa kuwa meneja bora wa mwezi wa 11 wa ligi kuu ya nchini Uingereza mara baada ya kuiongoza vyema klabu yake ya Newcastle kupata ushindi wa michezo mitatu kati ya minne aliyocheza ndani ya mwezi huo.
Pardew ameiongoza timu yake kupata ushindi wa 1:0 dhidi ya Liverpool kwenye dimba la St James' Park, kuwachapa klabu ngumu ya West Bromwich Albion kwa jumla ya magoli 2-0 kwenye dimba lao la nyumbani la the Hawthorns kabla ya kurejea nyumbani na kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Queens Park Rangers nyumbani kwao St James Park.
Kilicho nisukuma mimi kuandika makala hii ni hali ya mambo ilivyokua ndani ya klabu ya Newcastle miezi kadaa iliyopita pale ambapo mashabiki wa timu hiyo walikua wakiingia uwanjani wakiwa na mabango yanayowataka mabosi wa klabu hiyo kumfungashia virago meneja huyo nhio sababu iliyonifanya kichwa changu cha habari niseme
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni