Social Icons

Jumatano, 10 Desemba 2014

ASKOFU DESMOND TUTU ANASUMBULIWA NA TEZI DUME

Askofu Mkuu Mstaafu wa Cape Town, Desmond Tutu.
ASKOFU Mkuu Mstaafu wa Cape Town, Desmond Tutu, ameahirisha mipango ya ziara zake kwa mwaka mzima ujao kutokana na sababu za kiafya.
Taarifa iliyotolewa na taasisi yake imeeleza kuwa Askofu huyo ataanza matibabu hivi karibuni ili kukabiliana na tezi dume ambayo amedumu nayo miaka 15 iliyopita.
Binti wa Askofu huyo amemuelezea baba yake mwenye umri wa miaka 82, kwamba hatahudhuria tuzo za Nobel zitakazofanyika wiki hii huko Rome, Italia.(P.T)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates