Mwanariadha wa mbio za marathon raia wa Kenya Rita Jeptoo amegunduliwa kuwa alitumia dawa zinazosisimua misuli.
Shirika la riadha nchi Kenya limesema kuwa uchunguzi wa pili ulibaini kuwa mwanariadha huyo alitumia dawa hizo.
Shirika hilo linasema kuwa litasikiliza kesi hiyo mwezi Januari mwaka ujao .
Jeptoo alikuwa ameshinda mbio za Boston marathon mara tatu na za Chicago mara mbili na ni mmoja wa wanariadha maarufu zaidi nchini Kenya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni