1. Jifunze kuweka akiba ya fedha na iache bila kuigusagusa.
2. Tafuta mpenzi sahihi na tulia naye, panga maisha.
3. Ishi mahali pa peke yako, acha kuishi kwa wazazi au kupanga na nyumba na washkaji.
4. Lipa madeni yako ya zamani. Yote!
5. Tengeneza mwili ambao unataka halafu jitahidi kuu-maintain! Anza kuzingatia kuishi kwa kujali afya yako sana.
6. Jitahidi uwe na marafiki ambao wana changamoto za kimaendeleo zitakazokusaidia.
7. Anza kujinunulia assets kama ardhi na nyinginezo.
8. Jifunze kuvaa vizuri na kwa heshima, si tu ilimradi umependeza.
9. Kubali sasa kwamba umekua na acha tabia na mambo ya kitoto.
10. Yaache ya zamani yapite na anza mapya. Mwajuma huna mpango naye, achana naye. Acha kurudi rudi nyuma!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni