Social Icons

Alhamisi, 25 Desemba 2014

MAJONZI TELE! FAMILIA YALA KRISMASI NJE!


Familia hiyo ikiwa nje baada ya nyumba yao kuvunjwa. Stori: Deogratius Mongela na Chande Abdallah
Familia moja yenye makazi yake Mtaa wa Mwembe-Madafu, Ukonga jijini Dar, imejikuta ikila Sikukuu ya Krismasi na kulala nje kwa madai kwamba nyumba yao imevunjwa na baada ya kuuzwa kwa mtu mwingine na mwanafamilia anayetajwa kwa jina la Omary Hamisi ambaye ni mtoto mkubwa wa familia hiyo. 
Akizungumza kwa masikitiko makubwa mbele ya waandishi wetu, mmoja wa wanafamilia hao, Rajabu Hamisi (28) alisema kuwa historia ya nyumba hiyo ilianzia pale baba yao, Hamis Mangandali alipopewa na mzee mmoja aliyemtaja kwa jina la moja la Kombo mwaka 1961. 
Rajabu alisema kwamba, migogoro ilianza mwaka 1991 baada ya Bibi Kombo Mbwana (mmoja wa wanafamilia ya Kombo) alipomkabidhi nyumba hiyo baba yake, Hassani Ali aliyetajwa kama babu yao mzaa mama. Alisema kuwa babu huyo aliiuza nyumba hiyo kwa mtoto huyo mkubwa wa mzee Hamisi aitwaye Omari Hamisi kwa kiasi cha shilingi elfu sabini (70,000/=) bila wanafamilia wengine kufahamu.Rajabu aliongeza kwamba, mwaka 2012, familia yao ilishangaa kupokea notisi ikiwataka wahame nyumba hiyo kwa muda wa siku 14 kwa kuwa ilikuwa tayari imeuzwa.

Baadhi ya vitu vya familia hiyo vikiwa nje. “Tulishangaa lakini hatukuwa na namna. Tuliendelea kuishi kwenye nyumba.
“Kweli baada ya siku kutimia walifika watu wakatutupia virago nje. 

“Walipoondoka tukarudisha vitu ndani na kuendelea kuishi lakini kwa wasiwasi,” alisema Rajabu ambaye alidai kuwa sekeseke hilo lilijitokeza mwanzoni mwa mwezi huu hadi sasa.Alisema ukiachilia mbali kutupiwa vitu nje, nyumba hiyo ilivunjwa kabisa huku ndugu yao aliyedaiwa kuiuza akitowekea kusikojulikana. 

“Hadi sasa familia yetu yote ipo nje, si watoto wala baba wote tunakaa nje, mvua yetu, jua letu. Kimsingi sisi hatuna cha sikukuu wala nini,” alisema Rajabu na kuongeza kuwa kwa kipindi chote hicho wamekuwa hawamuelewi ndugu yao ambaye ameuza nyumba hiyo kuwa ana nia gani na familia yao hasa baba yao ambaye ni mzee. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates