Floyd Mayweather amethibitisha pambano lake na Manny Pacquiao litafanyika mwaka 2015
HATIMAYE bondia Floyd Mayweather Jnr ametaja Mei 2 mwakani kuwa tare he ya pambano lake na Manny Pacquiao.Tetesi juu ya ujio wa poambano hilo la utajiri mkubwa zimezidi kuenea tangu Pacman aonyeshe kiwango kizuri wakati anampiga Chris Algieri mjini Macau, China wiki mbili zilizopita.Sasa Mayweather, anazipa kazi ya ziada moja ya kampuni zake promosheni ya matukio kwa kusema: "Nitapigana na Pacquiao? Sahihi,".
Pacquiao (kulia) alimtaka Mayweather wapambane baada ya kumpiga Chris Algieri mwezi Novemba
Alipoulizwa litakuwa pambano lake lijalo, akajibu; "Sahihi," na alipotakiwa kutaja tarehe ya pambano lake lijalo, akasema; "Mei 2, sahihi,".
Bondia huyo ambaye hajapoteza pambano na anayesifiwa kwamba ndiye mkali wa kurupa makonde duniani ameongeza; "Watu wanalitaka hikli pambano. Nalitaka. Kikwazo pekee kilikuwa Bob Arum (promota wa Pacquiao) lakini nafikiri mabondia wote wanalitaka. Hivyo ni wakati wa kupambana,"amesema.
13 Dec 2014
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni