Social Icons

Alhamisi, 25 Desemba 2014

MAKOSA 6 KWENYE HOTUBA YA RAIS KIKWETE KUHUSU(ESCROW)

Hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa leo ina makosa zaidi ya 100 niliyoweza kuya-identify haraka, haya sita. 
1. Rais hakupaswa kutoa ufafanuzi kuhusu pesa ni za umma au sio za umma. Ufafanuzi huo ulishatolewa na PAC, CAG etc.. Yeye alitakiwa kuwawajibisha wote waliotajwa kuhusika.

 2. Suala la Escrow hakupaswa kuongea na wazee ambao wengi walikuwa hawaelewi kinachojadiliwa na walikua wakisinzia tu. Angetaka kueleweka angezungumza na wasomi wa chuo kikuu cha Dar (UDSM) au chuo kikuu kingine chochote. 

3. Si kweli kuwa pesa za Escrow hazikuwa za umma kama Rais anavyojaribu kusema.

4. Ikiwa si pesa za umma kwanini amemfukuza Tibaijuka? Unawezaje kumfukuza mtumishi aliyechukua fedha binafsi "in good faith" 

5. Ikiwa si fedha za umma kwanini ameunda kamati ya kuchunguza waliotuhumiwa? Unawezaje kuwachunguza watu waliochukua hela binafsi. Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!

6.Sheria ya Utumishi wa umma inataka kiongozi wa serikali akipewa zawadi inayozidi sh.50,000/= aikabidhi kwa tume ya maadili ya viongozi.. Tibaijuka amepewa Bil.1.6 (zaidi ya mara 34,000 ya kiwango kilichowekwa na sheria). Lakini Tume hiyo haijaona kuwa hilo ni kosa na haikumchukulia hatua yoyote mama Tibaijuka hadi Rais Kikwete alipochukua hatua jana. Hii ina maana kuwa Rais ameisaidia Tume ya maadili kufanya kazi yake. Kazi iliyopaswa kufanywa na tume imefanywa na Rais mwenyewe. Huu ni udhaifu. This means Tume iliona ni sawa Tibaijuka kubeba hela kwenye sandarusi/rambo/viroba etc, ndio maana ilikaa kimya hadi Rais alipoona ni kosa. sasa jana ilitakiwa Rais Kikwete kabla hajamfukuza kazi Tibaijuka aivunje kwanza Tume ya Ma-deal maana imeshindwa kazi.!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates