Baada ya Chelsea kupoteza mchezo kwenye ligi dhidi ya Newcastle jumamosi, Arsenal kudhalilishwa na Stoke City, huku Man City na Liverpool wakishinda – leo ilikuwa zamu ya Man United kucheza dhidi ya Southmpton.
Matokeo ya mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa St Mary umemalizika kwa United kushinda mechi ya 5 mfululizo na kufanikiwa kushika na nafasi ya tatu kwenye ligi, mara ya kwanza tangu Sir Alex Ferguson alipokuwa Kocha wao.
Magoli mawili ya Robin Van Persie yalitosha kuifanya United kuwaondoa West Ham katika nafasi ya 3.
Pelle aliifungia Southampton goli la
Kufutia machozi kwenye mchezo huo ambao United hawakucheza vizuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni