Maafisa wawili wa polisi mjini New York Marekani wameuawa kwa kupigwa risasi walipokuwa ndani ya gari lao eneo la Brooklyn.
Kamishna wa idara ya polisi mjini New York Bill Bratton amesema kuwa maafisa hao walilengwa na kuuawa kutokana na sare walizokuwa wamevaa.
Alisema kuwa awali mwanamume huyo alikuwa ameandika ujumbe wa kuwashutumu polisi kwenye mtandao wa kijamii baada ya kumfyatulia risasi na kumjeruhi vibaya mpenzi wake wa zamani .
Mauaji hayo ya polisi yanajiri wakati kunashuhudiwa ghadhabu kali kufuatia uamuzi wa hivi majuzi wa kutowafungulia mashtaka polisi wazungu waliohusika kwemye mauaji ya waamerika weusi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni