Social Icons

Jumatano, 24 Desemba 2014

UMEMUELEWA?DIAMOND AANIKA SABABU 5 ZA KUMPENDA ZARI.

Baada ya kutoka kimalavu na kumwagana na mwanadada mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kisha kuangukia kwenye ‘utamu’ wa penzi la mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameamua kuanika siri tano za kilichomvutia kwa staa huyo gumzo Afrika Mashariki.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady.
Akizungumza katika mahojiano maalum katika ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar hivi karibuni, bila kupepesa macho au kuuma maneno baada ya kuulizwa kinagaubaga juu ya ukaribu wake na Zari, Diamond au Dangote hakutaka kuficha, akaamua kuweka mambo yote hadharani.
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki mkubwa na mwenye heshima, wakati mwingine natakiwa kuwa na akili ya kuwa na uhusiano na watu ambao watakuwa msaada kwangu pia.
“Siwezi kuwa karibu na mtu ambaye hataniongezea kitu chochote kile. Baada ya kujitangaza sana Tanzania, nikahamia Kenya ambapo nilikuwa karibu na mwanadada Avril. Ukaribu wangu kwake, ukanifanya Kenya kutambulika.
“Baada ya kukaa kwa muda, nikataka nitambulike na Uganda pia, unafikiri ningefanya nini? Nikaliteka soko lao kwa kuwa karibu na mrembo Zari.
“Kweli nimefanikiwa na hata siku ya shoo yake (Desemba 18, mwaka huu nchini Uganda), ilikuwa ni balaa kiasi kwamba sikuamini kilichokuwa kimetokea, watu walikuwa nyomi ile mbaya. Mbali na kuwa mwanamuziki mkubwa, bado nahitaji kujitangaza zaidi.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates