Social Icons

Jumanne, 30 Septemba 2014

Ndege kubwa zaidi ya abiria duniani yaanza safari ndefu zaidi, angalia picha za ndani


Shirika la ndege la Australia linalofahamika kama Qantas limeanza kurusha ndege yake ambayo inatajwa kuwa kubwa zaidi ya abiria duniani na inayofanya safari zake kwa umbali mrefu zaidi.
Ndege hiyo iliyotwa kama Airbus A380 ilitua katika uwanja wa kimataifa wa Dallas-Fort Worth saa 15 tangu ilipoondoka Sydney, Australia safari ya Kilometer 13,805 ikiwa na abiria 480 .
Uwanja wa kimataifa wa Dallas- Fort Worth ni uwanja mkubwa wa ndege unaounganisha ndege zote za Marekani na Latin America. Uwanja huo umeonekana kufaa zaidi kwa ndege hiyo.


UEFA MATOKEO WAZEE WA KUBETI MPO?

Europe - UEFA Champions
League
FT CSKA Moskva 0 - 1 Bayern München
FT Manchester City 1 - 1 Roma
FT PSG 3 - 2 Barcelona
FT APOEL 1 - 1 Ajax
FT Sporting CP 0 - 1 Chelsea
FT Schalke 04 1 - 1 Maribor
FT Shakhtar Donetsk 2 - 2 Porto
FT BATE 2 - 1 Athletic Club

Hii kali.........................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Hii ishara inaonesha kuwa hautakiwi kunywa pombe .. sasa huyu jamaa anapata shida sana akitaka kunywa maji au chakula maana anatafuta kanafasi kadogo ili kufanya hivyo.
Ni alama ya tahadhali hii ni moja ya mamia ya watu ambao hawali nyama huko Thailand , huyu anaamini kwa kujiweka mapaga makali na kujichoma hivi itasaidia watu kuacha maovu kabisa na kuwapa amani mioyoni mwao
Hii ni hali ya kawaida sana kwao 
Huu ni utalii kabisa ambapo watu wengi wanaenda kuutazama , ikiwa kama kwetu pia likitokea kundi kama hili wanaokataa mambo maovu kwa mtindo huu itakuwa ni sehemu nzuri ya utalii
Hebu mtazame kwa umakini huyu jamaa yeye amejichoma na sindano kibao hapa chukua muda wako uzihesabu
Huyu kasha kula sana vyuma


Hii ni sema hapana kuto kula nyama, kufanya mapenzi na kunywa pombe 









Hii inamaanisha ni lazima kuangamiza maovu 




Haya si mapambo lakini hawa wanakataa matendo ya ajabu ajabu 






Sasa huyu ametobolewa na kuwekwa makamba mdomo mzima pia wanapigania kuacha na kutokomeza uhalifu 




Hapa Jibu unalo


Hapa wanaaminini nkabisa kwa kufanya hivi wanasema hapana kabisa uhalifu kataa uhalifu ndio maana yake hapa


Sasa Tazama huu Mjambia hapa jamaa analamba hajali vipi anaumia lakini anamaanisha uhalifu basi 




Tazama nanasi hizo zimepita katika waya ambao unasaidiwa na midomo yao ambauyo wamechomwa 





mambo yanaendelea 

Hapaana mchezo

MAGAZETI YA LEO


1_2f7e7.jpg

2_86b9d.jpg
34_da436.jpg6_03e6a.jpg 33_42b6f.jpg3_f4efd.jpg
30_f328a.jpg

4_7d9e2.jpg
36_3545b.jpg5_c598c.jpg

7_599c7.jpg
10_64c15.jpg
40_b9e51.jpg31_22721.jpg

Maandamano ya CHADEMA, UKAWA jijini Dar es Salaam

Wananchi wamefanya maandamano huko Manzese jijini Dar es Salaam wakipinga kile wanachokiita ni wizi unaoendelea ndani ya bunge Maalum la Katiba ikiwa ni mwendelezo wakutimiza tamko la Mwenyekiti wa CHADEMA na UKAWA la kufanya maandamano nchi nzima kupinga mchakato huo.

DROGBA WA PORI LA SELOUS ANAYEJIPATI MKWANJA MREFU KUTOKA KWA WAZUNGU

 Drogba 1KATIKA kipindi cha miaka minne iliyopita hadi kufikia leo, watalii wanaoenda kutembelea Pori la Akiba la Selous lililopo katika Kijiji cha Mloka kilichopo Kata ya Mwaseni wilayani Rufiji mkoani Pwani, wanapata fursa ya kufurahia utalii wa aina yake pindi wanapokutana na mmoja wa wanakijiji wa eneo hilo anayejulikana kwa jina la Mwananyika lakini kwa sasa amepewa jina la Drogba kutokana na umaarufu aliojipatia miaka ya hivi karibuni. Inaelezwa kuwa amefanana na Drogba yule mwanasoka anayechezea timu ya Chelsea kwa sasa.


Imeelezwa kuwa, Kijiji hiki ni kijiji cha mwisho kabisa kabla ya kufika kwenye geti la Mtemere, moja ya mageti ya kuingilia kwenye pori hili. Watalii kutoka ndani na nje ya nchi (hususani raia wa kigeni) wanapofika katika kijiji hiki hukutana na Drogba ambaye inaelezwa kuwa amepata umaarufu mkubwa kuanzia mwaka 2011 hadi sasa.
Drogba 2
Wenyeji wa kijiji hiki wanasema Drogba ni mmoja wa wajasiriamali aliyewekeza nguvu na uelewa wake wa mambo ya wanyama pori na mazingira yao kwa kutoe elimu kwa wageni wanaungana naye katika kuelewa tabia za wanyama. Yeye haingii kwenye hifadhi bali anazunguka nje ya pori hili kutokana na maeneo mengi kupitika kirahisi na wanyama kupata nafasi ya kuzunguka katika moja ya vijiji vilivyopo kijijini humo na maeneo ya jirani.
Yeye safari zake hujulikana kama bush walk na wageni wake hupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu maisha ya mwanakijiji na wanyamapori. Vitu kama dawa mbalimbali za asili, hadithi za kale huwa ni sehemu ya vitu wanavyojifunza wageni wa ‘Drogba’.
Shughuli za Mwananyika au Drogba
Watumiaji wa njia inayoelekea katika geti hilo wanaeleza kuwa moja ya shughuli anazofanya Drogba ni kuelekeza wageni kwenye matembezi wanaoingia kwenye pori hilo na kujipatia kipato cha kuendeshea maisha yake pamoja na familia yake (anatumia lugha tatu hadi sasa, Kiswahili, Kiingereza na Kifaransa).
Mwenyewe hujigamba kwa kuziita true Africa walking safari na anapokuwa kazini huwa anavaa mavazi ya asili kabisa (baadae huvaa mavazi ya kawaida) ambayo huyatengeneza kwa magome ya miti huku akiwa amebeba ngao, mkuki na kikapu chake cha kubebea mitishamba na vitu vingine anavyoweza kuvipata akiwa katika eneo lake la kazi pia anazunguka kwenye barabara zilizopo kando kando na pori hilo na wakati mwingine hulazimika kuingia kwenye baadhi ya mapori na kuzunguka na wageni wake nje ya hifadhi japo wapo wanyama (wakali na wapole) wapo katika maeneo anayotembelea.
Kwa ajili ya tahadhari na usalama anapofanya safari za miguu na wageni wake siku zote huwa anaambatana na Askari wa hoteli (campsite) waliofikia wageni wake, askari anakuwa na bunduki kwa ajili ya tahadhari kwa chochote kinachoweza kutokea.
Mara zote mgeni anayefanya utalii katika pori hili, husindikizwa na askari wa Maliasili na wakati huo Drogba yeye anaendelea kuzunguka nje ya hifadhi bila kuwa na woga.
Safari zake huwa na vituo vingi ndani yake na kwenye kila kituo kuna jambo ambalo huona ni vyema wageni wake wanastahili kulifahamu na pia endapo mnaweza kukutana na wanyama anatumia nafasi hiyo kuwafundisha wageni mazingira ya wanyama.
Miongoni mwa mambo wageni wanayofaidi wanapokuwa na Drogba ni kufundishwa namna ya kutambua nyayo za wanyama mbalimbali ambazo huwa wanakutana nazo wakiwa safarini.
Drogba
Historia yake kwa ufupi
Hadi sasa ukifika kijiji hicho kama mtalii ukasikia watu wanamzungumzia Drogba basi kuna uwezekano mkubwa wakawa wanamzungumzia Drogba wanayemjua wao anayetembeza wageni wanaotoka ndani nan je ya nchi. na sio yule ambaye watu mbalimbali wamemzoea kumsikia (anayechezea timu ya Chelsea).
Drogba Selous
Kwa hivi sasa watu wengi wanaeleza kuwa hata jina lake kamili hawalijui kutokana na umaarufu aliojipatia (ni mmoja kati ya watu maarufu sana kijiji hapo) na hususani kwa wadau wa utalii ambao hupeleka wageni kwenye pori hilo kupitia lango la Mtemere linalopakana na kijiji cha Mloka ambapo wanyama hutoka nje na kuzunguka vijijini na maeneo ya karibu.
Hali hii inawafanya wageni kufanya kutembelea maeneo ya nje ya pori ambazo huwaleta karibu na wanyama wa porini, baadhi ya wanyama wanaopatikana nje ya pori hilo ni Swala, Nyati,Tembo, Twiga na Viboko, na wanyama wengineo ambao huonekana katika maeneo ambayo Drogba hupendelea kuzunguka akiwa na wageni wake.
Ni nadra sana kuweza kumsogelea Twiga mpaka muwe na usawa wa karibu mara nyingi Drogba yeye anamkaribia bila Twiga kutimua mbio. Inaelezwa kuwa mara chache Twiga huvumilia kwa muda kidogo na baadae kuanza kulala akiwa na Drogba.
Unapoanza kukiacha kijiji cha Mloka na kisha kuelekea lilipo geti la kuingilia Selous (Mtemere) utaanza kukutana na vibao vikikuonyesha zilizopo kambi kadhaa. Kambi nyingi za Mloka zimejengwa pembezoni mwa mto Rufiji ukiwa unaelekea Mtemere nyingi zipo upande wa Kushoto wa barabara

KALI YA LEO UMOJA WA MA-GIRLFRIEND TZ WAMEKUJA NA HII BAADA YA ZAWADI ALIZOPEWA WEMA SEPETU


September 26 ilikua ni siku ambayo mrembo kutoka Tanzania Wema Sepetu alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ndani ya siku yake hii ukitoa party aliyoifanya kulikuwa na vitu mbalimbali vya kuvutia. Siku hiyo Diamond platnumz aliamua kumzawadia zawadi ya gari mpenzi wake Wema Sepetu gari aina ya Nissan Murano ambapo alipost instagram na kuandika maneno yafuatayo yaliyoambatana na picha ya zawadi hiyo. 
 
Mbali na zawadi aliyoitoa 
September 26 ilikua ni siku ambayo mrembo kutoka Tanzania Wema Sepetu alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ndani ya siku yake hii ukitoa party aliyoifanya kulikuwa na vitu mbalimbali vya kuvutia. Siku hiyo Diamond platnumz aliamua kumzawadia zawadi ya gari mpenzi wake Wema Sepetu gari aina ya Nissan Murano ambapo alipost instagram na kuandika maneno yafuatayo yaliyoambatana na picha ya zawadi hiyo. 
Diamond Platnumz ya gari hilo pia Meneja wake Martin Kadinda nae alimpatia Wema Sepetu zawadi ya Gari aina ya BMW mpya kabisa ikiwa na namba mpya za sasa.

Sasa baada ya zawadi hizo kuonekana eti umoja wa Ma-Girlfriend Tanzania nao wameamua kutoa Ya moyoni kwa Ma-Boyfriend wao kuhusu birthday zao inapofika muda wa kusherehekea,hiki ndicho walichokiandika.

ANGALIA VIUMBE WENYE MADHARA MAKUBWA SANA KWA BINADAMU


 










 
 
Blogger Templates