Shirika la ndege la Australia linalofahamika kama Qantas limeanza kurusha ndege yake ambayo inatajwa kuwa kubwa zaidi ya abiria duniani na inayofanya safari zake kwa umbali mrefu zaidi.
Ndege hiyo iliyotwa kama Airbus A380 ilitua katika uwanja wa kimataifa wa Dallas-Fort Worth saa 15 tangu ilipoondoka Sydney, Australia safari ya Kilometer 13,805 ikiwa na abiria 480 .
Uwanja wa kimataifa wa Dallas- Fort Worth ni uwanja mkubwa wa ndege unaounganisha ndege zote za Marekani na Latin America. Uwanja huo umeonekana kufaa zaidi kwa ndege hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni