Social Icons

Jumatatu, 8 Septemba 2014

RAIS WA UEFA ATISHIA KUMUADHIBU RIBERY ASIPOICHEZEA UFARANSA


Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), Michel Platini amesema Bayern Munich italazimika kutoa adhabu ya kumsimamisha Franck Ribery kucheza mechi tatu iwapo atagoma kuichezea Ufaransa.

Riberry ametangaza kustaafu kuichezea Ufaransa akisisitiza ni wakati wa kuwaachia vijana.Lakini Platini ambaye ni nyota wa zamani wa Ufaransa amesema mwenye chaguo la kucheza au la ni kocha, kwamba amtumie yupi lakini mchezaji hawezi kukataa kuichezea timu ya taifa kama ameitwa.
Kocha wa Les Bleus (Ufaransa), Didier Deschamps amemchagua Ribery kwenye kikosi chake.

'[Kwa Ribery] hana uwezo wa kuamua kujiunga au kutojiunga na timu ya taifa kama kocha wake Didier Deschamps amemuita.
'Hii iko wazi kwenye kanuni za Fifa, kama akikataa basi Bayern Munich wanatakiwa kuchukua hatua. Mimi hata simuelewi, Michuano ya Ulaya itafanyika Ufaransa mwaka 20I6,” alisisitiza Platini.

Kauli hiyo ya Platini imeonyesha kuwashitua wengi na hasa kuhusiana na suala la kumlazimisha mchezaji kujiunga na timu ya taifa wakati alijiuzulu kwa hiari yake.
Ribery alikosa michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil wakati Ufaransa ilipotolewa kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil kutokana na kuwa majeruhi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates