Taaarifa kutoka syria zinasema zaidi ya watoto kumi na mbili wamekufa na wengine kuugua baada ya kupewa chonjo ya surua inayosemakana kuwa haukuwa salama katika eneo linalodhibitiwa na waasiShirika la Uingereza linahusika na uangalizi wa haki za binadamu nchini Syria limesema chanjo hiyo ilitolewa katika maeneo ya vijijini kaskazini mwa Syria.Ugonjwa kama surua na polio umesambaa tangu kutokea kwa mafarakano miaka ya 2011.
Huduma za afya zimevurugika sana nchini Syria.
Wapinzani kutoka chama Syrian National Coalition wa nchi hiyo wamesema watasitisha mpango wa chanjo ya surua kufuatia vifo hivyo vilivyotokea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni