Shinji Kagawa akishangilia baada ya kuifungia Borussia Dortmund bao tangu arudi klabuni hapo
SHINJI Kagawa amefurahia ndoto za kurudi Bundesliga kufuatia kiungo huyo wa zamani wa Manchester United kufunga bao moja na kutengeneza moja katika mechi yake ya pili akiichezea Borussia Dortmund.Nyota huyo wa kimataifa wa Japan, alimtengenezea Adrian Ramos bao lake la kwanza katika dakika ya 34 dhidi ya Freiburg, kabla ya kufunga la pili kabla ya mapumziko.
Kagawa alikaribishwa vizuri ambapo alisalimiwa na mabango na bendera za Japan.
Nyota wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa (kulia) akishangilia bao lake katika uwanja wa Westfallonstadion
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni