Social Icons

Jumamosi, 6 Septemba 2014

ARTURO VIDAL AKANUSHA KUUMIA GOTI


1409940926273_wps_12_image001_png
Niko kamili gado: Kiungo wa Juventus, Arturo Vidal amekunusha ripoti zinazodai ameumia tena.
KIUNGO wa Juventus,  Arturo Vidal amejibu mapigo kuhusu taarifa za kupata majeruhi tena kwenye goti lake akiwa katika majukumu ya kimataifa na Chile.
Ripoti zilieleza kuwa Vidal, ambaye alihusishwa kujiunga na Manchester United majira ya kiangazi mwaka huu, aliondoka mazoezini mjini Miami baada ya kuumia goti kwa mara nyingine.
Hata hivyo, Vidal kupitia akaunti yake ya Twita amekanusha taarifa hizi akisema alikuwepo muda wote katika mazoezi ya timu hiyo.
Wanted man: The Chile midfielder was linked with a move to Manchester United during the summer
“Goti langu liko sawa,” Vidal aliandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii. “Tafadhali acheni kuzusha taarifa. Njooni Chile”.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alifanyiwa upasuaji wa goti mwishoni mwa msimu uliopita na alionekana kutokuwa fiti sana katika fainali za kombe la dunia.
Majeruhi imemuathiri Vidal katika haraka zake za kujijenga kuwa miongoni mwa viungo bora wa dunia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
 
Blogger Templates